LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Aug 25, 2021

ATEMBELEA FAMILIA YA MAGUFULI NA MKAPA NCHINI TANZANIA

 

   Aliyekuwa waziri mkuu nchini Kenya Raila Odinga hii leo amezitembelea familia za marais wa zamani nchini Tanzania Hayati John Pombe Magufuli na Benjamin Mkapa.

Raila ambaye hapo Jana alihudhuria sherehe za kuapishwa kwa rais mpya wa Zambia Hakainde Hichilema alipiga picha na wake za marais hao wawili wakiwa nyumbani kwao.

Katika chapisho lake la twitter Raila amesema:

‘’Nimepita ili kutembelea familia za rafiki zangu rais Benjamin Mkapa na John Magufuli. Nafurahia kukutana na Anna Mkapa na Janeth Magufuli wakiwa katika hali nzuri’’.

Baadaye alimaliza kusema:

‘’Mungu azilaze roho zao mahali pema peponi’’

Kiongozi huyo amekuwa rafiki wa karibu wa viongozi hao wawili waliofariki na hususan John Pombe Magufuli kabla na hata alipokuwa rais wa Tanzania na hatmaye kifo chake.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages