LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 6, 2021

SEKRETATIETI YA CCM IKIONGOZWA NA KATIBU MKUU CHONGOLO YAKUTANA NA KUZUNGUMZA NA RAIS DK. MWINYI, IKULU ZANZIBAR, JANA.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo akimkabidhi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mjumbe wa Kamati Kuu (CC) ya CCM Dk. Hussein Ali  Mwinyi barua ya Pongezi kwa kazi nzuri ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM Zanzibar, kama ilivyoelekezwa na Halamshauri Kuu (CC) ya CCM katika kikao cha tarehe 29 Juni 2021 kilichofanyika jijini Dodoma. Alimkabidhi barua hiyo alipokwenda Zanzibar na Sekretarieti ya CCM kujitambulisha baada ya uteuzi wao uliofanyika Aprili 30, 2021. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Abdallah Juma Mabodi na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Christina Mndeme.
Katibu Mkuu wa CCM Daniel Chongolo (aliyesimama) alipokuwa akijitambulisha na kuwatambulisha wa Wajumbe wa Sekretarieti kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Dk. Hussein Ali Mwinyi, Ikulu jijini Zanzibar, jana. Kushoto ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka, Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Abdallah Juma Mabodi na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Christina Mndeme.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Dk. Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza kwa makini Katibu Mkuu wa CCM Daniel Chongolo wakati Katibu Mkuu huyo akijitambulisha na kutambulisha Wajumbe wa Sekretarieti ya CCM, Ikulu jijini Zanzibar, jana.
Katibu Mkuu wa CCM Daniel Chongolo (aliyesimama) alipokuwa akiendelea kujimbulisha na kuwatambulisha wa Wajumbe wa Sekretarieti kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Dk. Hussein Ali Mwinyi, Ikulu jijini Zanzibar, jana.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Dk. Hussein Ali Mwinyi akiwa katika mazungumzo na Katibu Mkuu wa CCM Daniel Chongolo na Wajumbe wa Sekretarieti ya CCM, baada ya mazungumzo yao, Ikulu jijini Zanzibar, jana.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Dk. Hussein Ali Mwinyi akiwa katika picha ya kumbukumbu na Katibu Mkuu wa CCM Daniel Chongolo na Wajumbe wa Sekretarieti ya CCM, baada ya mazungumzo yao, Ikulu jijini Zanzibar, jana. Kushoto ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya UWT Queen Mlozi, Katibu wa NEC, Uchumi na Fedha Dk. Frank Hawasi, Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga, Katibu Mkuu wa UVCCM Kenan Kihongozi na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Christina Mndeme. Kutoka kulia ni Katibu wa Sekretarieti ya CCM Salum Reja, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi Erasto Sima, Katibu wa NEC Oganaizesheni Moudline Castico na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Abdallah Juma Mabodi.

©CCM Blog/2021

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages