Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Mradi Kabambe wa Kusambaza Umeme Vijijini, Awamu ya Tatu, Mzunguko wa Pili, Mkoa wa Mara, uliofanyika katika kijiji cha Kitunguruma, Kata ya Mbaribari, wilayani Serengeti, Julai 8 mwaka huu.
Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Amos Maganga, akipunga mikono kuwasalimu wananchi wa kijiji cha Gibaso, Kata ya Kwihancha, wilayani Tarime, Mkoa wa Mara, ambapo Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani (hayupo pichani) alisimama kuzungumza nao baada ya kuzindua Mradi Kabambe wa Kusambaza Umeme Vijijini, Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili, Ngazi ya Mkoa, uliofanyika katika kijiji cha Kitunguruma wilayani Serengeti
Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani akizungumza na wananchi wa kijiji cha Gibaso, Kata ya Kwihancha, wilayani Tarime, Mkoa wa Mara, baada ya kuzindua Mradi Kabambe wa Kusambaza Umeme Vijijini, Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili, Ngazi ya Mkoa, uliofanyika katika kijiji cha Kitunguruma wilayani Serengeti
Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani akimtambulisha kwa wananchi Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Amos Maganga (kulia), wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi wa Mradi Kabambe wa Kusambaza Umeme Vijijini, Awamu ya Tatu, Mzunguko wa Pili, Mkoa wa Mara, uliofanyika katika kijiji cha Kitunguruma, Kata ya Mbaribari, wilayani Serengeti
Mbunge wa Tarime Vijijini, Mwita Waitara (kulia), akimkaribisha Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani kuzungumza na wananchi wa kijiji cha Gibaso, Kata ya Kwihancha, wilayani Tarime, Mkoa wa Mara, ambapo Waziri alisimama kuzungumza nao baada ya kuzindua Mradi Kabambe wa Kusambaza Umeme Vijijini, Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili, Ngazi ya Mkoa, uliofanyika katika kijiji cha Kitunguruma wilayani Serengeti
Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani akiwatambulisha wakandarasi, Kampuni ya Gizal Cable Industries Ltd, watakaotekeleza Mradi Kabambe wa Kusambaza Umeme Vijijini, Awamu ya Tatu Mzunguko wa Kwanza, Mkoa wa Mara. Waziri alizindua rasmi Mradi huo Ngazi ya Mkoa katika kijiji cha Kitunguruma wilayani Serengeti
Wananchi wa Kijiji cha Kitunguruma, Kata ya Mbaribari, wilayani Serengeti, Mkoa wa Mara, wakimsikiliza Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi wa Mradi Kabambe wa Kusambaza Umeme Vijijini, Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili, Ngazi ya Mkoa, uliofanyika katika kijiji hicho
Wananchi wa Kijiji cha Gibaso, Kata ya Kwihancha, wilayani Tarime, Mkoa wa Mara, wakimsikiliza Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani (hayupo pichani) aliyesimama kuzungumza nao baada ya kuzindua rasmi Mradi Kabambe wa Kusambaza Umeme Vijijini, Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili, Ngazi ya Mkoa, katika hafla iliyofanyika katika kijiji cha Kitunguruma, Kata ya Mbaribari, wilayani Serengeti, Julai 8, 2021.
………………………………………………………………..
Veronica Simba na Hafsa Omar – Mara
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuvunja rekodi kwa Marais wote wa Afrika katika uunganishaji umeme vijijini.
Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani amebainisha hayo wakati akizungumza na wananchi katika hafla ya uzinduzi wa Mradi Kabambe wa Kusambaza Umeme Vijijini, Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili, Ngazi ya Mkoa, iliyofanyika katika kijiji cha Kitunguruma, Kata ya Mbaribari, wilayani Serengeti, Mkoa wa Mara, Julai 8 mwaka huu.
Akifafanua, Dkt. Kalemani alieleza kuwa Tanzania inatarajiwa kuandika historia ya kuunganisha umeme katika vijiji vyote vya Tanzania Bara ifikapo Disemba 2022 hivyo kuongoza katika Bara la Afrika kufikia mafanikio hayo.
“Tulianza utekelezaji wa miradi hii katika ngazi ya wilaya, kisha vijiji ambapo hadi sasa zaidi ya vijiji 10,312 vimeshapelekewa umeme; na vilivyobakia takribani vijiji 1,956 ndivyo vinapelekewa katika mradi huu,” alibainisha Waziri.
Akieleza zaidi, Dkt Kalemani alisema mafanikio hayo makubwa yametokana na uongozi mzuri wa Rais Samia ambaye Serikali anayoiongoza imedhamiria kwa dhati kuleta maendeleo kwa wananchi.
Awali, akielezea utekelezwaji wa Mradi huo katika Mkoa wa Mara, Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Amos Maganga, alibainisha kuwa utagharimu takribani shilingi bilioni 9.63
Aidha, aliongeza kuwa Mradi umelenga kuvifikishia umeme vijiji 45 vya Mkoa huo ambavyo ndivyo pekee vilivyosalia kati ya vijiji vyake vyote 459.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti, Mbunge wa Serengeti Amsabi Mrimi na Mbunge wa Tarime Vijijini Mwita Waitara, waliipongeza Serikali kwa kazi nzuri ya usambazaji umeme vijijini na kuahidi kuwa wananchi wao wako tayari kupokea umeme na kuutumia kwa shughuli za maendeleo.
Hafla hiyo ya uzinduzi ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, vyama vya siasa na wananchi.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇