Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi, Robert Gabriel, pamoja na Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa NMB , Alex Mgeni wakifurahia jambo baada ya uzinduzi rasmi wa Klabu ya Madini ya ‘NMB Mining Club’ kwa Kanda ya Ziwa. Kushoto ni Kaimu Meneja wa NMB Kanda ya Ziwa, Dickson Richard na Rais wa Shirikisho la wachimba Madini, John Bina.
Sehemu ya wageni waalikwa ambao ni miongoni mwa wachimba madini wa Kanda ya Ziwa wakiwa katika hafla ya uzinduzi wa NMB Mining Club uliofanyika katika hotel ya Gold Crest- Mwanza.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi, Robert Gabriel akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa ‘ NMB Mining Club’ kwa Kanda ya Ziwa.
Benki ya NMB imepanga kutumia zaidi ya Sh.120 bilioni
kutoa mikopo ya mitaji, vifaa na mitambo kwa wachimbaji wadogo wa madini kuunga
mkono juhudi za Serikali za kuongeza tija katika Sekta ya Madini nchini. Akizungumza
jijini Mwanza wakati wa uzinduzi wa Klabu la Wachimba Madini Kanda ya ziwa,
(NMB Mining Club) Mkuu wa Idara ya Biashara wa NMB, Alex Mgeni alisema hadi sasa,
tayari benki hiyo imetoa mikopo yenye thamani ya zaidi ya Sh.63 bilioni kwa
kundi hilo.
“Wachimbaji wadogo watakopeshwa vifaa na mitambo bila
kulazimika kuweka dhamana kwa sababu mitambo na vifaa hivyo ndivyo vutakuwa
dhamana yao baada ya kulipa kuanzia asilimia 20 ya thamani ya kifaa au mtambo
anaotaka kununua,” alisema Mgeni.
Akizuzugumza wakati wa hafla hiyo iliyoshirikisha
wachimbaji zaidi ya 200 kutoka mikoa ya Mwanza, Mara, Simiyu, Geita, Shinyanga
na Kagera, Rais wa Shirikisho la Wachimba Madini Tanzania (Femata), John Bina
alisema uamuzi wa benki ya NMB kuanzisha dirisha la mikopo kwa Sekta ya Madini
siyo tu utaongeza tija, bali pia utakuza uchumi wa wachimbaji na Taifa kwa
ujumla.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Robert Gabriel aliihakikishia
NMB utayari wa Serikali wa kushirikiana na taasisi za fedha na wadau wengine
kutekeleza sera na mikakati ya kuongeza tija katika sekta ya madini aliyosema
imekuwa kwa kasi ndani ya kipindi cha miaka mitano iliyopita.
Aliwashauri wachimbaji wadogo nchini kuunganisha nguvu
kimtaji kumudu siyo tu kufungua migodi ya kati na mikubwa, bali pia kutoa
huduma katika migodi mikubwa ya Kimataifa kupitia sera ya local content
inayoelekeza sehemu ya huduma migodini kutolewa na kampuni za wazawa
Kuhusu
“NMB Mining Club ni mpango unaolenga kufikia miji sita nchini yaani Mwanza,
Chunya, Morogoro na Arusha, ulianzia Dodoma na Kahama na maeneo ya karibu kwa
lengo la uwezeshaji na kutoa mafunzo ya biashara, elimu ya mwendelezo wa kitaalamu wa madini) na fursa ya
kukutana na kubadilishana uzoefu wa kibiashara.. Ubunifu
huu ndio unaoifanya NMB kuendelea kuwa kinara wa huduma na bidhaa katika sekta
ya kibenki
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇