Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa NMB, Alex Mgeni akipokea bidhaa zilizosindikwa na Mjasiliamali, Doroth Kimati anayewezeshwa na NMB katika uzinduzi wa Klabu ya " NMB Mwanamke Jasiri" jijini Mwanza. Katikati ni Mjasiliamali, Hellen Bugoye.
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Amina Makilagi, akizungumza wakati akizindua Klabu ya NMB Mwanamke Jasiri jijini Mwanza.
Baadhi ya akina mama wajasiriamali wakifuatilia hotuba mbalimbali kwenye uzinduzi wa Klabu ya NMB Mwanamke Jasiri jijini Mwanza.
Mkuu huyo wa wilaya aliyasema hayo alipokuwa
anazungumza na umati wa wanawake na wakazi wengine wa mkoa huo waliohudhuria uzinduzi
wa klabu ya ‘mwanamke jasiri’ mkoani Mwanza na Kanda ya Ziwa kwa ujumla.
Bi. Makilagi alisema kuwa wakazi wa Mwanza wasiache
kuchangamikia fursa zinazoletwa na benki ya NMB kwani benki hiyo ina malengo
mazuri ya kutaka kuleta maendeleo kwa wateja wake.
AidhaMkuuhuyowa wilaya aliwasihi sana wanawake
kutoogopa kuchukua mikopo ya NMB kwaninimikoporafikisananamasharti yake sio
magumu kabisa.
Akizungumza katika uzinduzi huo, Mkuu wa Kitengo cha Biashara
kutoka Benki ya NMB, Alex Mgeni alisema lengo la kuzinduaKlabuhiinikuzidi kumpa
ujasiri mwanamke na wao kama benki kupata fursa ya kutoa mafunzo ya fedha kwa
wanawake ilikuwaongoza vyema katika ukuaji wao kiuchumi.
Bw. Alex aliongeza kuwa ndani ya mwaka mmoja, benki
hiyo imefanikiwa kutoa mikopo ya bilioni 100 kwa wanawake zaidiya 8000 Mkoani Mwanza hukuakiwakaribisha wateja wengine
kufika ili kujipatia mikopo kwa manufaa yao.
Uzinduzi huo uli hudhuriwa na wateja na
wafanyabiashara wa benki ya NMB matawi ya Igoma, Ilemela, Buzuruga, Mwanza
Business Centre, Kenyatta, Rock city naPambaRoad, yote yajijini Mwanza.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇