LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 2, 2021

MADAKTARI WATAKAOWAHAMISHA WAGONJWA KWA HILA KWENDA HOSPITALI BINAFSI KUKIONA-NAIBU WAZIRI DKT MOLLEL+video

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,  Dkt.Godwin  Mollel akizungumza na vyombo vya habari jijini Dodoma leo Julai 2, 2021 wakati wa Kikao Kazi na wakurugenzi na mameneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) wa kutathmini utendaji na uboreshaji wa huduma za mfuko na wateja wao pamoja na watoa huduma walioingia nao mkataba. Kushoto ni .Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Bernard Konga

Dkt. Mollel amesema kuwa Serikali itawachukulia hatua kali madaktari watumishi wa Hospitali za Umma wanaowahamisha kwa hila wagonjwa kutoka hospitali za umma kwenda hospitali za binafsi kwa lengo la kujipatia kipato zaidi.

Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Bernard Konga akitoa rai kwa watoa huduma wasiowaaminifu kuacha mara moja tabia hiyo na kwamba watakaobainika watachukuliwa hatua kali ikiwemo kuzifuta leseni zao na kuvifuta vituo vyao.
Baadhi ya wakurugenzi na mameneja wa  NHIF, wakiwa katika kikao kazi cha siku mbili kinachoongozwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt Godwin Mollel.



Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii ya video, Naibu Waziri Dkt. Mollel na Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Konga wakielezea juu ya tatizo hilo.......
 

 

Imeandaliwa na Richard Mwaikenda

 Mhariri Blog ya Taifa ya CCM 

0754264202

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages