LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 14, 2021

LUKUVI KUTEMBELEA MITAMBA KESHO JULAI 15

WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, ndugu William Lukuvi (pichani) kesho anatarajia kutembelea eneo la mitamba, Mtaa wa Lumumba, Kata ya Pangani, Kibaha Mjini Mkoani Pwani.
Eneo hilo la Mitamba ni mali ya Serikali na lilikuwa likitumika kwa ajili ya kulishia mifugo, lakini sasa limeuzwa na baadhi ya viongozi wasio waaminifu, huku wakiwashawishi waliowauzia waseme wamevamia ili waonewe huruma na Serikali.
Baadhi ya wananchi hata hivyo wanahoji je ni kwanini eneo livamiwe wakati kuna viongozi wa Serikali ambao wanalo jukumu la kulinda mali za Serikali, je ni ardhi gani ya kiongozi iliyovamiwa na yeye kiongozi akaiachia watu wavamie? Jibu ni hakuna.
Wananchi waliozungumza na Blogu hii wanasema imani yao ni kuwa Waziri Lukuvi atalirudisha eneo hilo Serikalini ili litumike kujenga viwanda ambavyo vitasaidia kuharakisha maendeleo ya nchi kwa jamii kupatiwa ajira na bidhaa mbalimbali kuendelea kupatikana kwa urahisi zaidi.
“Hakuna aliyevamia hapa Mitamba, bali tumeuziwa na baadhi ya viongozi wa Serikali za mitaa na kata. Ushauri wangu kwa Waziri Lukuvi ni kwamba waliouziwa maeneo warudishiwe fedha au kutafutiwa maeneo mengine na wale waliowauzia, Serikali ichukue eneo hili kwa ajili ya maendeleo ya nchi ikiwamo kuweka wenye viwanda” anasema mkazi mmoja wa Mtaa wa Lumumba, Jamiel Khalfan.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages