****************
Na Ahmed.Mahmoud,Arusha
Mkuu wa Jeshi la
Polisi Nchini,IGP ,Simon Sirro amewataka wenyeviti wa serikali za
mitaa,watendaji kata na vijiji kuwa macho kwa kuwatambua wageni
wanaoingia katika maeneo yao ili kuepusha nchi kuingia kwenye matukio ya
ugaidi na uhalifu.
Aidha ameagiza
kata zenye changamoto za matukio ya uhalifu ,ubakaji,watoto kutelekezwa
au matukio mengine zitapelekewa askari polisi ili kuweza kudhibiti
matukio hayo.
Akizungumza jana
Jijini Arusha na watendaji kata,wenyeviti wa serikali za mitaa,viongozi
wa dini,polisi jamii pamoja na viongozi mbalimbali wa serikali,IGP Sirro
alisisitiza lazima wenyeviti hao wahakikishe amani na utulivu unakuwepo
katika jamii
“Nasema hivi
kwasababu hapa Arusha ni eneo hili limepakana na nchi jirani hivyo
kuingia kwa wageni wasio na nia njema na nchi yetu ni rahisi hivyo ni
lazima kila mmoja awe makini na wageni hao ili tusirudi miaka iliyopita
ya mabomu katika maeneo mbalimbali”
Aliwataka
viongozi hao kutanguliza maslahi ya Taifa na wananchi badala ya maslahi
yao kwa kuwa mstari wa mbele kufichua wahalifu na uhalifu unaofanyika
katika maeneo yao
Aidha Sirro
alibainisha kuwa kata zenye changamoto mbalimbali ikiwepo kata ya
Olasiti ili kukomesha matukio ya kiuhalifu yanayojitokeza ni vema kukawa
na polisi kata kwaajili ya kutatua kwa haraka changamoto zinazowakabili
wananchi wa eneo hilo
Pia aliagiza
mikutano ya kila mwezi Kati ya Mkuu wa Polisi Wilaya(OCD) na viongozi
wa ngazi mbalimbali za chini kwaajili ya kupeana taarifa za matukio
mbalimbali na kuzitatua kwani uhalifu unaanzia majumbani,mitaani na
maeneo mengine
“Tunahimiza
ushirikiano na wananchi juu ya ulinzi shirikishi kwani bado polisi ni
wachache ukilinganisha na watanzania waliopo hivyo ushirikiano ni muhimu
katika kufichua na kukomesha matukio ya kiuhalifu”
Pia IGP Sirro
aliwaonya wanaojiingiza katika matukio ya uhalifu na ugaidi kuacha mara
moja kwani endapo watahusika katika katika uhalifu watashughulikiwa kama
wahalifu wengine”
Akizungumza
kuhusu madawa ya kulevya alisema Arusha ni Mkoa wa pili kwa uuzaji wa
madawa ya kulevya hivyo ni aibu na lazima hatua zichukuliwe ili
kudhibiti matukio hayo ambapo alisisitiza doria zitaimarishwa zaidi
katika maeneo husika ili kudhibiti suala hilo la madawa ya kulevya haswa
katika kata ya Ungalimited
Awali Mkuu wa
Wilaya ya Arusha,Sophia Mjema alisisitiza umuhimu wa ulinzi na usalama
ngazi za chini ni lazima ili kuleta maendeleo katika kila kata na
serikali za mitaa
Wakati huo
huo,Mbunge wa Arusha Mjini,Mrisho Gambo alisema Arusha ni Jiji la Utalii
lakini huwezi kufanya utalii bila kuwa na amani usalama na kusisitiza
lazima ulinzi uimarishwe.
Wakati huo.huo
IGP Sirro ametoa sh, milioni 5 na Gambo sh, milioni 5 kwaajili ya ujenzi
wa kituo cha Polisi cha Olasiti huku Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Dk
John Pima akiahidi kumalizia vituo vingine vya polisi kwaaajili
kudhibiti matukio ya uhalifu.
Kata ya Olasiti
ni miongoni mwa kata ndani ya jiji la Arusha zinazokabiliwa na matukio
mengi ya kiuhalifu ikiwemo ubakaji wa watoto na wanawake pamoja na
matukio mengine ya uhalifu
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇