LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 8, 2021

900 WASAJILIWA NHIF MAONESHO YA SABASABA





 Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

JUMLA ya wanachama 900 wamesajiliwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya na wananchi 2,500 wamepata huduma ya elimu ya umuhimu wa bima ya afya katika Maonesho ya SabaSaba tangu yaanze Juni 28 mwaka huu.

NHIF inashiriki maonesho hayo katika viwanja vya Mwalimu Nyerere, Dar es Salaam ambapo huduma mbalimbali zinatolewa ikiwemo ya elimu, usajili wa wanachama pamoja na kupokea maoni na kutatua changamoto zinazowakabili wanachama.

Akizungumzia mwitikio wa wananchi kufika bandani hapo, Meneja Uhusiano wa NHIF, Bi. Anjela Mziray amesema kuwa, wananchi wamekuwa na mwitikio mkubwa katika kufika na kupata huduma za elimu na kujiunga ili wanufaike na mafao yanayotolewa.

“Tangu maonesho haya yaanze tumeshahudumia zaidi ya wananchi 2,500 kwa kuwapatia elimu na tumesajili jumla ya wanachama wapya 900 wakiwemo watoto chini ya umri wa miaka 18 na waliojiunga kupitia mpango wa vifurushi,” alisema Bi. Mziray.

Alisema kuwa Mfuko umejipanga kuwahudumia wananchi hivyo wajitokeze na wafike katika banda la Mfuko ambalo liko nyuma ya banda la Jakaya Kikwete. “Tuko hapa mpaka Julai 13, mwaka huu hivyo wananchi watumie fursa hii kufika na kujiunga.


Akizungumzia huduma zinazotolewa na Mfuko, aliwahakikishia wanachama wapya wanaojiunga kuwa, Mfuko umesajili zaidi ya vituo 9,000 vilivyopo Tanzania Bara na Zanzibar lakini pia watanufaika na kitita cha mafao kilichoboreshwa kwa kuzingatia huduma zote za msingi  kwa mwanachama.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages