LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jun 30, 2021

ZIARA YA MWENYEKITI WA UWT MKOA WA DAR ES SALAAM NA KAMATI YA UTEKELEZAJI, ILIVYOTIKISA UBUNGO, JANA

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Florence Masunga akipokea zawadi ya mbuzi kutoka kwa viongozi wa UWT na CCM Wilaya ya Ubungo, kumpongeza wakati wa Mkutano wa ziara yake na Kamati ya Utekelezaji na Viongozi wa ngazi mbalimbali wa UWT na (CCM),  Wilaya ya Ubungo, uliofanyika jana, katika Ukumbi wa Victory Geneses, Temboni wilayani humo. Kushoto ni Katibu wa UWT mkoa huo Grace Haule.

Kisha wakampa na kadi kubwaaa! ya pongezi. Grace Haule (Kushoto), yeye wampa zawadi ya kitenge.

Baada ya utoaji zawadi, zikalipuka shangwe la kusakata wimbo wa "Wanawake na Maendeleo.."👇😀






Mwisho wa Shangwe👏👏

Mkutano ukaendelea👇
Viongozi meza kuu wakiwa wamesimama baada ya kuwasili ukumbini.
Katibu wa UWT Ubungo Mary Miwa akishauriana jambo na kiongozi mwenzake kabla ya kusimama jukwaani kwenye kikao hicho.
Katibu wa UWT Wilaya ya Ubungo Mary Miwa (kulia) akizungumza mambo kadhaa na kumkaribisha Mwenyekiti wake kuzungumza kwenye mkutano huo.
Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Ubungo Pili Mustapha akizungumza kumkaribisha Katibu wa UWT mkoa kuhutubia.
Katibu wa UWT mkoa wa Dar es Salaam Grace Haule akizungumza katika mkutano huo.
"Wanawake lazima ifikie mahali tujitambue wote kuwa tunastahili kugombea nafasi zote za uongozi, ndani na nje ya UWT , sasa mwaka wa uchaguzi ndani ya Chama unawadia, tusilale, tujitokeze kugombea", akasema kwa msisitizo Katibu Grace Haule.
Katibu wa UWT mkoa wa Dar es Sallaam Grace Haule akisisitiza jambo kwenye mkutano huo.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ubungo Ndugu Mgonja akizungumza kwenye mkutano huo.
Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Dar es Salaam Florenge Masunga akihutubia wakati akihutubia kwenye mkutano huo
Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Dar es Salaam Florenge Masunga akisisitiza jambo wakati akihutubia kwenye mkutano huo.
"Hivi ndivyo nyumba tunazowajengea watumishi wetu wa UWT mkoa wa Dar es Salaam, zitakavyokuwa", akisema Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Dar es Salaam, Florence (kulia), wakati akizungumzia ujenzi wa nyumba hizo ambazo ni sita.
Mwenyekiti wa UWT tawi la Mbezi Madukani, Mbezi Hidaya Mambosasa (Katikati), akiwa na wenzake Wakati Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Dar es Salaam akihutubia.
Wajumbe wakiwemo Madiwani wakimsikiliza Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Dar es Salaam wakati akiwahutubia.
Wajumbe wakimsikiliza Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Dar es Salaam wakati akiwahutubia.
Wajumbe wakiwa wamefurika ukumbini kumsikiliza Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Dar es Salaam wakati akiwahutubia.
Kina mama wa UWT wa upande wa kikosikazi cha mkutano huo wakiwa wamepumzika ukumbini huku wakisikiliza hotuba
Viongozi meza Kuu wakiwa amesimama wakati wa dua ya kubariki kikao Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Dar es Salaam alipokuwa hajaanza kuhutubia
Wajumbe wakiwa amesimama wakati wa dua ya kubariki kikao Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Dar es Salaam alipokuwa hajaanza kuhutubia
Mwenyekiti wa UWT tawi la Mbezi Madukani, Mbezi Hidaya Mambosasa, akiwa amesimama na wenzake Wakati Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Dar es Salaam hajaanza kuhutubia.
"Mkuu, hapo vipi? Naona kama shughuli imefana" ni kama ndivyo alivyokuwa akisema Katibu wa UWT mkoa wa Dar es Salaam Grace Haule (kushoto) kumnong'oneza Mwenyekiti wake Florence mwishoni mwishoni mwa kikao hicho.
Vijana wa UVCCM wakikusanya data za michancho ya ujenzi wa nyumba za watumishi wa UWT uliofanyika wakati wa kikao hicho
Mamaa Mashauzi Aisha Ramadhani, ambaye aliwania Ubunge kupitia UWT naye hakuwa mbali, hapa akipigwa picha na Mwentekiti wa UWT na Katibu wa UWT mkoa wa Dar es Salaam.
Kisha Katibu wa UWT mkoa wa Dar es Salaam, Grace Haule akahitimisha mkutano huo kwa kuzungumza na Waandishi wa Habari kuhusu shughuli yote.
"Hongera Katibu wetu bora wa UWT mkoa, ziara imenoga", akisema, Kada wa CCM Kindakindaki, Nuru Mhina ambaye Katibu wa UVCCM Goba, wakati akimpongeza Katibu wa UWT mkoa wa Dar es Salaam Grace Haule baada ya mkutano huo. Sasa tazama mtiti wa kuserebuka kwenye clip hii ifuatayo👇
Picha naVideo vimetayarishwa na Bashir Nkoromo, Msimamizi Mkuu wa Blog hii ya Taifa ya CCM (CCM Blog). Kwa mawasilino piga 0712498008 au 0789498008, Karibu.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages