Dodoma, jana.
Akizungumza Alhamisi 24 Juni 2021 kupitia jukwaa la walimu waliofanya ziara ya kimafunzo makao makuu ya CCM Dodoma, Katibu Halmashauri Kuu ya Taifa Itikadi na Uenezi, Ndg. Shaka Hamdu Shaka, amesema Serikali ya CCM inatambua na kuthamini mchango mkubwa unatolewa na walimu nchini katika kuelimisha, kuwaandaa na kulea vyema vijana hivyo kipaumbele cha serikali ya awamu ya sita ni kuhakikisha sekta hiyo inamarika.
"Mhe Rais Samia baada wanafunzi 11,000 kukosa mikopo elimu ya juu, ameongeza billioni 70 ili kuwanufaisha walikosa waendelee mikopo na ameongeza bujeti ya billioni 300 kwa bodi ya mikopo ili waweza kutoa huduma kwa wanafunzi wengi zaidi. Chama kitafutilia kwa karibu ili kuona ufanisi wake katika kuondoa vilio na malalamiko kwa wanafunzi." Alisema Shaka.
Amefahamisha kuwa serikali ya CCM imeendelea kutekeleza ilani uchaguzi 2020/2025 kwa kuboresha mazingira ya watumishi nchini ikiwemo walimu ambapo serikali imepunguza kodi “payee” kutoka asilimia 9 ya awali hadi asilimia 8, Lakini pia serikali ya CCM imetoa ajira kwa walimu 6000 na imeelekeza watumishi wote wenye sifa wakiwemo walimu wapandishwe madaraja na kulipwa malimbikizo yao yote jambo ambalo uratibu wake unaendelea.
Aidha Katibu Mwenezi ametoa Rai kwa walimu nchini kutoa elimu juu ya matumizi mazuri ya mitandao ya kijamii kwa vijana, sambamba na kuendelea kuwajengea uzalendo na kutambua thamani ya utaifa wao.
Viongozi wa Jukwa la walimu wako katika mafunzo ya Siku mbili mkoani Dodoma ambapo pia wamepata fursa ya kutembelea maeneo mbali mbali kujifunza shuhuli za uendeshaji wa taasisi husika.
Picha mbalimbali kuhusu tukio hilo👇
Imeandaliwa na Idara ya Itikadi na Uenezi CCM HQ
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇