LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jun 25, 2021

MAOFISA WA KITENGO CHA DHARURA NEMC WATEMBELEA MTAA WA MAKUKA KUSINI KATA YA MBAGALA KUU

Katibu wa Kamati ya wananchi Ryoba Mginga (katikati aliyeshika kablasha mkononi) akizungumza na baadhi ya Maofisa kitengo cha Dharura kutoka Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) akishirikiana na viongozi Serikali ya Mtaa Makuka Kusini Kata ya Mbagala Kuu mara walipo fika Ofisini hapo kwa lengo la kujionea maeneo yaliyoathiriwa na maji yanayo daiwa na Wananchi kuelekezwa katika makazi yao na kujionea nyumba zilizo bomoka kutokana na maji hayo Juni 24, 2021. (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)

Midomo 3 ya maji inayolalamikiwa na Wananchi kuelekezwa katika meneo ya makazi kama inavyo onekana pichani

Mkazi wa Mtaa wa Makuka Kusini Kata ya Mbagala Kuu Lukas Liendeko akizungumzia athari aliyoipata katika midomo ya maji iliyoelekezwa katika makazi ya watu na pamoja na kutumia gharama zaidi ya Milioni 2 na nusu anaomba kufidiwa gharama hizo ambapo mazao na miti ilisombwa na pamoja na kugomea Serikali haikutaka kuwasikiliza Wananchi 
Maofisa kitengo cha Dharura kutoka Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kwa kushirikiana na viongozi Serikali ya Mtaa Makuka Kusini Kata ya Mbagala Kuu wakielekea kwenye maeneo ya makazi ya watu yanayo daiwa kuathiriwa na maji yaliyo elekezwa kutoka Barabara ya Kilwa na kujionea maeneo yaliyoathiriwa na maji katika makazi ya watu na kujionea nyumba zilizo bomoka kutokana na maji hayo na kushoto ni Katibu wa Kamati ya wananchi Ryoba Mginga.
Baadhi ya nyuma zinazo diwa kufikiwa na maji mpaka katika mfereji wa Barabara.
Katibu wa Kamati ya wananchi Ryoba Mginga akiwaonyesha moja ya nyumba ambayo maji huwa yakifika katika nyumba hiyo pamoja na kijiwekea msingi mkubwa. 

Mjumbe Serikali ya Mtaa Mwanamtoti Radhia Ramadhani (kushoto) akizungumza na Maofisa kutoka Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) wakiwemo na Viongozi Mbalimbali wa Mtaa huo wakizunguuka katika meneo yalitoathiriwa na maji yanayodaiwa kuelekezwa maeneo ya nyumba za makazi ambapo nyumba kadhaa wamejionea ambazo zilizo athirika na mji hayo.
  Kaimu Mwenyekiti Serikali ya Mtaa wa Makuka Kusini Haji Malenda (kushoto) akizungumza na Mmoja wa Maofisa hao kutoka Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) mara walipo fika Ofisini hapo kwa lengo la kujionea maeneo yaliyoadhiriwa na maji yanayodaiwa kuelekezwa katika makazi ya watu na kujionea nyumba zilizo bomoka kutokana na maji hayo.

Maofisa kutoka Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) wakishirikiana na Viongozi wa Serikali ya Mtaa wakizungumza jambo baada ya kujionea nyumba yenye familia 3 wakiishi katika nyumba hiyo huku ikiwa imezingirwa na maji kwa nyakati hizi mvua imezimama
Maofisa kutoka Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) wakizungumza jambo na viongozi wa mtaa wa Makuka Kusini.
Mkazi wa Mbagala Kuu Rebeka Mozes akipita kwa umakini mkubwa katika Daraja hilo lililojengwa kwa miti na Wananchi.
Katibu wa Mbunge Jimbo la Mgagala (katikati) ambaye jina lake halikupatikana mara moja akizungumza jambo mara baada ya kufika katika maeneo ya makazi ya watu na kujionea madhara yaliyotokana na maji yanayodaiw kuelekezwa kwao. 
Maofisa kutoka Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) wakipita katika Daraja lililojengwa kwa miti na kujionea maeneo yaliyoathiriwa na maji yanayoelekezwa katika makazi ya watu na kujionea nyumba zilizo bomoka kutokana na maji hayo









Moja ya Baadhi ya nyumba iliyopitiwa na maji yatokayo Barabara ya Kilwa yanayo daiwa kuleta madhara kwa Jamii wa wakazi ya watu wa Mtaa wa Makuka Kusini 
Moja ya Baadhi ya nyumba iliyopitiwa na maji yatokayo Barabara ya Kilwa yanayo daiwa kuleta madhara kwa Jamii wa wakazi ya watu wa Mtaa wa Makuka Kusini 
Moja ya Baadhi ya mdomo wa maji unaodaiwa na wananchi kusababisha madhara ya watu na malizao ukiwa umeelekezwa katika Mtaa wa Makuka Kusini 
Mjumbe Serikali ya Mtaa Mwanamtoti Radhia Ramadhani (kushoto) akiangalia mdomo wa maji ulioelekezwa katika Mtaa wake huku akishuhudiwa na wananchi kwake 
Afisa Mtendaji Mtaa wa Makuka Kusini Isdory Ngosha (wakwanza kulia) akizungumza jambo mara Maofisa kitengo cha Dharura kutoka Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kufika maeneo wanyolalamikiwa na wannchi
Katibu wa Kamati ya wananchi Ryoba Mginga (kushoto) akizungumza jambo mara walipo fika katika shimo kubwa lenye midomo mitatu Barabara ya Kilwa  inayo daiwa kuelekezwa katika Makazi ya watu 
Katibu wa Kamati ya wananchi Ryoba Mginga (kushoto) akizungumza jambo mara walipo fika katika shimo kubwa lenye midomo mitatu Barabara ya Kilwa  inayo daiwa kuelekezwa katika Makazi ya watu

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages