LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jun 17, 2021

RAIS WA KWANZA WA ZAMBIA DK. KENNETH KAUNDA AFARIKI DUNIA MJINI LUSAKA, LEO

Dk. Kenneth Kauda


Lusaka, Zambia

Rais wa kwanza wa Zambia, Dk. Kenneth David Buchizya Kaunda amefariki dunia leo, Juni 17, 2021 mjini Lusaka nchini humo.


Taarifa za awali zimesema Dk. Kaunda ambaye amefariki akiwa na umri wa miaka 97 amefikwa na umauti akiwa katika Hospitali ya Maina Soko jijini Lusaka alikokuwa amelazwa tangu siku chache zilizopita.


Dk. Kaunda alilazwa katika hospitali hiyo ya Kijeshi kufuatia kuzidiwa na maradhi yaliyokuwa yanamsumbua kwa siku kadhaa ambayo hata hivyo hayajatajwa.


Mwanasiasa huyo Dk. Kaunda aliyezaliwa April 28, 1924, aliitawala Zambia kuanzia mwaka 1964 hadi mwaka 1991.


"Zambia’s first President and our founding father, Dr Kenneth David Buchizya Kaunda He passed away in Lusaka today, after a short illness.


We express our deepest condolences to the Kaunda family during their bereavement and pray for strength as they come to terms with this sad loss.


KK will be sorely missed by all Zambians and the rest of the people on the African continent"

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages