LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jun 18, 2021

RAIS SAMIA ATANGAZA SIKU SABA ZA MAOMBOLEZO YA KITAIFA YA KIFO CHA DK. KAUNDA, ATUMA SALAM ZA RAMBIRAMBI KWA RAIS WA ZAMBIA

Hayati Dk. Kenneth Kaunda
 
Ikulu, leo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Samia Suluhu Hassan, ametangaza siku saba za maombolezo ya Kitaifa hapa nchini kufuatia kifo cha Rais wa kwanza wa Zambia, Dk. Kenneth David Kaunda, kilichotokea jana mjini Lusaka Zambia. 

Taarifa iliyotolewa leo na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Jafar Haniu imesema, katika kipindi hicho cha maombolezo, bendera zote zitapepea nusu mlingoti.

Imesema, Rais Samia ametuma salamu za rambirambi kwa Rais wa Zambia, Edgar Chagwa Lungu, familia ya marehemu  na wananchi wote wa Zambia kwa kumpoteza kiongozi wao.

Rais Samia amemtaja Hayati Dk. Kaunda kuwa miongoni mwa viongozi mahiri na jasiri kuwahi kutokea barani Afrika, ambapo wakati wa uhai wake alitoa mchango mkubwa kwenye harakati za ukombozi wa Bara la Afrika kwa kushirikiana na viongozi wengine, akiwemo Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Vilevile, Hayati Dk. Kaunda alikuwa miongoni mwa waanzilishi wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).

"Tanzania itamkumbuka Hayati Dk. Kaunda kwa mchango wake katika kukuza uhusiano na ushirikiano kati ya mataifa yetu mawili, ambao uliwezesha kutekelezwa kwa miradi mikubwa ya kimkakati, ikiwemo Mamlaka ya Reli kati ya Tanzania na Zambia (TAZARA) na Bomba la Kusafirisha Mafuta (TAZAMA).

Mwenyezi Mungu aipumzishe roho yake mahali pema Peponi", taarifa hiyo imesema, ikimnukuu Rais Samia.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages