Wakazi wa Kakonko Mkoani Kigoma wameiomba serikali kuharakisha ujenzi wa hosipitali ya Wilaya ili kupunguza usufumbufu wa kusafiri kwenda mbali pale wanapokuwa wamepewa Rufaa ya kupata huduma za Hospitali kutokana na wilaya hiyo kutokuwa na Hosipitali.
Wananchi haoa mbao ni Fausta Mussa na Felista Kagoloba wameyasema hayo jana baada ya kuhudhuria ziara ya ukaguzi wa Miradi ya maendeleo unaofanywa na Kamati ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kigoma ambapo wamesema huduma hiyo wamekuwa wakiifuata Bukombe Geita, Biaharamulo Kagera na Kibondo.
‘’Tmekuwa tukipata adha kubwa hasa pale inapotakiwa kufuata huduma za hospitali wakati mwingine fedha hatuna au ni kidogo japo hapa huduma zingine za hospitali zinapatikana kwenye kituo cha afya Kakonko ambacho ndo tunakitazama kama hospitali ya wilaya na pia tunaishukuru serikali kwa kuanza ujenzi wa hospitali alisema Felista.
Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Masumbuko Magangila alisema ujenzi huo unatarajia kukamilika julai30 2021 na kueleza kuwa kulikuwa na changamoto ya mvua iliyonyesha mfululizo mwezi April ambapo alisema Majengo mawilai ya awali ujenzi uko 75% na Majengo 5 yako 45% ya ujenzi.
Jumla ya miradi 5 imekaguliwa na kamati hiyo ambayo ni ujenzi wa Zahanati ya Luhulu, Standi ya Mabasi, Hospitali, Mradi wa Maji Kiziguzigu, na Barabara za Mjini ambapo Katibu wa Ccm Mkoa wa Kigoma Kajolo Vyoholoka amewataka watendaji wa halmashauri ya Kakonko kuendelea na kasi iliyopo na kuendeleza mshikamano.
Aidha Kajolo alisema wao Kama chama watashauri ili fedha zinazobaki bila kuletwa ziweze kutumwa kwa wakati ili kusaidia kukamilisha miradi hiyo na kupongeza hatua mbalimbali za zilizofikiwa katika ujenzi wa miradi hiyo.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya hiyo Venance Malasa amesema mwaka 2020/21 walipokea sh 3.1 bilion kwa ajili ya miradi mbalimbali zilizokwishatumika ni 2 bilion na kuwataka Wananchi kuendelea kushirika katika ujenzi wa miradi inayoibuliwa katika maeneo yao ili kuondoa changamoto ya upatikanaji wa huduma hasa maeneo ya Vijijini.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇