LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jun 24, 2021

KATIBU MKUU UVCCM KIHONGOSI KUFANYIWA MAPOKEZI RASMI KESHO JIJINI DODOMA, ZIJUE BAADHI YA SIFA ZAKE

Katibu Mkuu wa UVCCM Kenani Kihongosi.


Na Bashir Nkoromo, CCM Blog

Katibu Mkuu mpya wa Umoja wa Vijana wa Chama Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Kenani Kihongosi anatarajiwa kufanyiwa mapokezi rasmi kesho, Juni 25, 2021 kwenye Makao Makuu ya CCM jijini Dodoma.


Kihongosi aliteuliwa kushika wadhifa huo katika Kikao cha Kamati Kuu ya CCM kilichofanyika juzi jijini Dodoma chini ya Mwenyekiti wa CCM Rais Samia Suluhu Hassan.


Baadhi ya Wasifu wa Kenani ni huu hapa👇

- Amekuwa Waziri Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Iringa.


- Amekuwa Katibu Mkuu Mtendaji wa Jumuiya ya vyuo vikuu Tanzania TAHLISO.


-Amekuwa mjumbe wa Kamati ya Siasa Tawi.


-Mjumbe wa Kamati ya siasa Kata.


-Mjumbe Halmasahuri Kuu ya Wilaya.


-Mjumbe wa Kamati ya siasa ya Mkoa.


-Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Mkoa.


-Mjumbe wa Baraza Kuu UVCCM Taifa.


-Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa.


-Amewahi kugombea udiwani akakosa.


-Akagombea Uenyekiti UVCCM wilaya akakosa.


- Akagombea Uenyekiti wa UVCCM mkoa akapata.


-Akaenda China kuwakilisha mkutano wa kiuchumi wa Vijana 2018.

- Akateuliwa kukimbiza Mwenge wa Uhuru Kitaifa.

-Akateuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Arusha, baadae Akateuliwa tena kuwa DC Wilaya ya Iramba.

Na sasa ni Katibu Mkuu wa UVCCM

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages