UYUI, Tabora
Mkuu wa Wilaya ya Uyui mkoani Tabora Kisare Makori amewataka wale wote wanaohusika kusimamia sekta ya Tumbaku kila mmoja kuwajibika vizuri ili zao hilo liweze kuleta tija na kuinua hali ya uchumi wa wananchi katika Wilaya hiyo na mkoa wa Tabora kwa jumla.

Kisare ametoa agizo hilo alipofanya ziara ya kustukiza katika ghala la Ex TTB kukagua mwenendo wa mauzo ya tumbaku.
"Nawaombeni kwa dhati, wale wote wanaohusika kusimamia sekta hii ya zao la Tumbaku kila mmoja wetu kusimamia ipasavyo.
Vipo Vyama vya Msingi vya AMCOS, Bodi ya Tumbaku, lakini pia tunao wafanyabiashara wetu kama hawa Kampuni ya Alliance tuliofanya nao muamala hapa Kwa Mtumba, kila mmoja atekeleze wajibu wake ipasavyo ili kuleta tija kwenye zao hili", amesema Makori.
Amesema, zao la Tumbaku likisimamiwa vizuri litainua hali ya Uchumi wa wananchi wa wilaya ya Uyui na mkoa wa Tabora kwa jumla, kwa kuwa asilimia 85 ya wananchi wa wilaya hiyo wanategemea zao hilo la tumbaku na zao hilo ndiyo dhahabu ya Uyui na mkoa huo wa Tabora.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇