LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

May 13, 2021

WIZARA YA MALIASILI NA UTALII YAFUNGUA MILANGO MIPYA YA UWEKEZAJI KATIKA MAENEO YA UHIFADHI NCHINI

Dodoma, Tanzani

Wizara ya Maliasili na Utalii imefungua milango mipya katika Sekta ya Utalii nchini kwa kutia saini ya  Uwekezaji wa kimkakati katika  maeneo ya Uhifadhi nchini kwa Wawekezaji wenye mitaji mikubwa wa kutoka ndani na nje ya nchi.


Ameyasema hayo leo Jijini Dodoma, Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Damas Ndumbaro   wakati akitia saini  kanuni za Uwekezaji wa kimkakati katika maeneo ya Uhifadhi nchini.


Waziri wa Maliasili na Utalii amesema utiaji saini huo ni miongoni mwa  njia  zitakazochangia kuongeza idadi ya Watalii kufika milion 5  na mapato yapatayo bilion 6 ifikapo mwaka 2025 kupitia Sekta ya Utalii nchini.


Kwa mujibu wa Kanuni hizo Wawekezaji wataweza kuwekeza katika maeneo ya Mapori ya Akiba, Mapori Tengefu pamoja na Maeneo ya Wazi ya Wanyamapori kwa miaka isiyopungua 25.


Akizungumza kabla ya utiaji saini huo, Waziri Dkt.Ndumbaro amesema kanuni hizo zimelenga Wawekezaji wenye mitaji mikubwa ambao hata watalii watakaokuja katika maeneo hayo ni Watalii wenye fedha nyingi ikiwemo watu maarufu duniani.


Amesisitiza kuwa kanuni hizo zitawezesha Wawekezaji hao kujenga mahoteli katika maeneo ya Uhifadhi pamoja na kuweka miundombinu ya Utalii itakayosaidia kuwavutia Watalii wengi kutembelea katika maeneo hayo.


Awali amesema kanuni hizo ni mpya na uwekezaji huo katika maeneo hayo utakuwa wa aina yake kwa vile umelenga Wawekezaji wenye mitaji mikubwa watakaowavutia Watalii matajiri hali itakayopelekea pato la taifa kuongezeka maradufu kupitia sekta ya utalii nchini.


Awali Mwenyekiti wa Bodi ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania ( TAWA) Meja Jenerali ( Mstaafu)  Hamis Semfuko amesema utiaji saini wa kanuni  ni moja ya hatua muhimu ya kupanua fursa zitokanazo na sekta ya utalii nchini.


" Tuliamua kuja na wazo hili ili Wawekezaji wenye mitaji mikubwa waweze kuwekeza katika maeneo ya Uhifadhi ambapo awali uwekezaji wa namna hii ulikuwa hauwezekani" alisisitiza Mwenyekiti huyo Meja Jenerali ( Mst) Semfuko

 

Kwa upande wake , Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt.Allan Kijazi amesema atahakikisha Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, ( TFS ) nao wanasaini kanuni za namna hiyo nao waweze kuwavutia Wawekezaji kuwekeza katika maeneo yao kwa vile wa maeneo yenye sifa kawa yalivyo ya TAWA.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Damas Ndumbaro akisaini kanuni za Uwekezaji wa Kimkakati katika maeneo ya Uhifadhi nchini, leo jijini Dodoma. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Sheria Lucy Saleko kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii na kukia ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mary Masanja  wakishuhudia utiaji saini huo.



Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania ( TAWA) Meja Jen ( Mstaafu) Hamisi Semfuko akizungumza kabla ya hafla ya utiaji saini Kanuni za Uwekezaji wa Kimkakati katika maeneo ya Uhifadhi ambapo amesema anatarajia Uwekezaji huo utaongeza mapato Serikalini kwa vile unalenga Wawekezaji wakubwa.


Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt.Allan Kijazi akizungumza kabla ya kumkaribisha Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro wakati wa hafla ya Utiaji saini wa Kanuni za Kimkakati za Uwekezaji katika maeneo ya Uhifadhi nchini ambapo amesema Wameanza na TAWA lakini na TFS pia  wana maeneo kama hayo ambayo yanahitaji kanuni hozo ili Uwekezaji uweze kufanyika 


Kamishna Uhifadhi wa TAWA, Mabula Misungwi akiwa  Kamishna Msaidizi wa Biashara na Huduma za Utalii kutoka TAWA  wakifuatilia utiani Saini wa Kanuni za Uwekezaji wa Kimkakati katika maeneo ya Uhifadhi nchini uliofanyika leo Jijini Dodoma.

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages