Rais wa chama Cha Wauguzi Alexander Baluhya akizungumza jambo wakti wa Maadhimisho y Siku ya Wauguzi Duniani yaliyo fanyika Mkoani Manyara Mei 12, 2021.
Mkurugenzi Huduma za Uuguzi na Ukunga, Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jisia Wazee na Watoto Dodoma. Ziada Sellah akizungumza jambo katika Maadhimisho ya Wauguzi yaliyofanyika Mkoani Manyara Kitaifa Mei 12, 2012/
Mkurugenzi wa Tiba Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dakt. Grace Magembe akizungumza jambo wakati wa Sherehe ya Wauguzi iliyo fanyik Mkoani Manyara
Mkuu wa Mkoa Joseph Mkirikiti akizungumza jambo wakati wa Sherehe ya Wauguzi iliyo fanyika Mkoani Manyara katika Kiwanja cha Kwaraa Mkoani humo
Katibu Mkuu wa Chama cha Wauguzi Sebastian Luziga akisom Risala ya Chama wakati wa Maadhimisho ya Wauguzi Duniani yaliyofanyika Mkoani Manyara Mei 21, 2021.
Rais wa chama Cha Wauguzi Alexander Baluhya (kushoto) akiteta jambo na Mgeni rasmi, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Ummy Mwalimu wakati wa Maadhimisho ya wauguzi kitaifa yaliyofanyika Kiwanj cha Kwaraa Mkoni Manyara
Baadhi ya Wauguzi Wastaafu wakito Burudani
Baadhi ya Viongozi na Wananchi wakimsikiliza Waziri Ummy alipokuwa akizungumza na Wauguzi hao Mkoani Manyara. Wa pili kushoto ni Mwenyekiti U.W.T (W) Babati. Claudina Hauli
Msani Chap Chap (Fadhili Mungi) akifikisha Ujumbe wa Wauguzi kwa Mhe. Ummy Mwalimu
Wauguzi wakiwa wanawasha mishumaa kwa ajili ya kula Kiapo chao cha Uuguzi kama ilivyo ada kwa kujikumbusha kila ifikapo Mei 12, ya Kila mwaka
Wauguzi wakila Kiapo katika Kiwanja cha Kwaraa, Wa (kwanza kulia) ni Mkurugenzi wa Uuguzi Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam, Zuhura Maona
Baadhi ya Viongozi wa kiwa jukwaani wakimsikiliza Waziri Ummy alipokuwa akizungumza na Wauguzi Mkoani Manyara, kulia ni Katibu Tawala Mkoa wa Manyara . Missaile Musa
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Ummy Mwalimu akimkabidhi Cheti Mwenyekiti wa TANNA Mkoa wa Manyara na Mratibu wa Afya ya Uzazi na Mtoto Halmashauri ya Wilaya Babati ambapo kwa sasa ni Mstaafu. Yasinta Msangi wakati wa Sherehe ya Wauguzi iliyofanyika Mkoani Manyara. kulia ni Mkuu wa Mkoa Joseph Mkirikiti
Pichani ni Wauguzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili na Mloganzila
Mkuu wa Mkoa Joseph Mkirikiti akimkabidhi zawadi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Ummy Mwalimu zawadi iliyoandaliwa na Chama cha Wauguzi (TANNA)
Nteghenjwa Hosseah, Manyara
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Ummy Mwalimu amesema Wauguzi ni miongoni mwa wataalamu wa Afya wanaopaswa kuheshimiwa na kupewa thamani inayostahili na wasichukuliwe kisiasa.
Waziri Ummy ameyasema hayo wakati alipokuwa akihutubia kwenye maadhimisho ya siku ya Wauguzi Duniani yakiyofanyika Mkoani Manyara Mei 21 ,2021.
Amesema Uuguzi ni fani adhimu na kuwataka viongozi wa Mikoa na Wilaya kuacha kuwadhalilisha kwa kuwaweka ndani kwa tuhuma zisizo na ushahidi.
“Viongozi wa Mikoa na Wilaya niwatake kuelewa kuwa uuguzi ni taalamu adhimu na muache kuamuru wawekwe ndani au kuwachukulia hatua kali ambazo haziendani na taalum yao kwa tuhuma ambazo hazina ushahidi, hili tuliache mara moja,”amesema.
Ameongeza "Kama Muuguzi amekosea akashitakiwe kwenye Baraza la Wauguzi na Wakunga ambapo atachukuliwa hatua kwa matakwa ya taaluma yake na sio kwa utashi wa kisiasa.”
Hata hivyo, amesema kiongozi yeyote atakayemuweka ndani muuguzi awe amethibitisha ameiba lakini kwa tuhuma nyingine akashitakiwe kwenye Baraza lao la Kitaaluma.
Pia Mhe.Ummy amewataka Wakurugenzi wa Halmashauri kuacha kuwakatalia wauguzi kwenda kusoma mara wanapopata fursa za kwenda kujiendeleza kielimu.
"Wauguzi lazima wathaminiwe kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kuhudumia wagonjwa sababu mara zote ukienda hospitali Daktari atakuona kwa muda mchache sana na wakati mwingi utakuwa na nesi katika kukuhudumia hivyo wapewe moyo,"amesema.
Amewapongeza na kuwashukuru Wauguzi kwa kazi kubwa walioifanya wakati wa wimbi la ugonjwa wa Corona na amewataka kuendelea kutimiza wajibu wao na kuokoa maisha ya watu.
Akijibu hoja zilizowasilishwa na Wauguzi katika risala yao, Waziri Ummy amesema suala la muundo linafanyiwa kazi na lilishawasilishwa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma kwa hatua zaidi.
Mhe. Ummy amesema kwa sasa Madaktari na wauguzi wafanye kazi kama timu moja ili kuleta matokeo chanya kwa jamii inayowategemea na hayo ya kiutawala yataendelea kuangaliwa na kufanyiwa kazi.
Kuhusu posho ya majukumu, amesema Ofisi ya Rais TAMISEMI itaangalia ni namna gani inaweka mazingira bora kwa wauguzi walioko TAMISEMI kwa kadri rasilimali zitakavyopatikana.
"Ofisi yangu itahakikisha inatoa kipaumbele katika kutatua changamoto ya uhaba wa nyumba za watumishi wa Afya kwa kujenga nyumba za kutosha ili watumishi hao waweze kukaa kwenye vituo vyao na kufanya kazi kwa amani,"amesema.
Katika hatua nyingine, Mhe. Ummy ametoa zawadi ya sh.500,000 kwa Muuguzi Aldolefina Shayo
wa Zahanati ya Kilangare iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Same ambaye amevunja rekodi ya kuhudumia wagonjwa hamsini kwa siku bila kunung’unika na leo ameshindwa kushiriki maadhimisho hayo kwa kuwa yuko peke yake kwenye zahanati hiyo na hakuna mtu wa kumsaidia.
Waziri Ummy amesema katika ajira mpya zilizotangazwa watapelekwa wauguzi wawili na Mganga mmoja ili kuboresha zaidi huduma za Zahanati hiyo.
Mwenyekiti wa TANNA Mkoa wa Manyara na Mratibu wa Afya ya Uzazi na Mtoto Halmashauri ya Wilaya Babati ambapo kwa sasa ni Mstaafu, Yasinta Msangi wa pili kushoto akimkabidhi Bango la Chama Makamu wa Chama cha Wauguzi Tanzania (TANNA). Ibrahim Mgoo, mara baada ya kumalizika sherehe hiyo ya Wauguzi ambapo mwakani zitafanyikia Kilimanjaro
Wauguzi wakipita mlele ya Mgeni rasmi katika Kiwanja cha Kwaraa Mkoani Manyara
Wauguzi wakiwa katika maandamno wakipita mlele ya Mgeni rasmi Waziri Ummy Mwalimu katika Kiwanja cha Kwaraa Mkoani Manyara
Wauguzi wakiwa katika maandamno wakipita mlele ya Mgeni rasmi Waziri Ummy Mwalimu katika Kiwanja cha Kwaraa Mkoani Manyara, aliye jifunga kitambaa chekundu kichawani ni Mkurugenzi wa Uuguzi Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam, Zuhura Maona
Mkurugenzi Huduma za Uuguzi na Ukunga, Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jisia Wazee na Watoto Dodoma. Ziada Sellah (kushoto) akifuatilia jmbo huku akiwa na Mkurugenzi wa Tiba Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dakt. Grace Magembe na kulia ni Naibu Waziri wa Habari Sanaa, Utamaduni na Michezo na Mbunge wa Babati Mjini. Pauline Gekul.
Wauguzi ya Hospitali ya Taifa Muhimbi na Mloga Nzila wanogesha Sherehe ya Wauguzi Mkoani Manyara
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇