Na Allawi Kaboyo, Biharamulo.
Mgodi wa Madini wa Stamigold uliopo wilayani Biharamulo Mkoani Kagera unatumia zaidi ya Sh. Bilioni 1.2 kwa mwezi kwaajili ya kununulia mafuta aina ya Diesel Ili kuweza kuendesha Mitambo ya uchimbaji na uchenjuaji wa Madini.
Kauli hiyo imetolewa na Meneja mkuu wa Mgodi huo Mhandis Gilay Charles Shamika Mei 19, mwaka huu mbele ya Mbunge wa Jimbo la Biharamulo Magharibi Mhe. Mhandis Ezra Chiwelesa alipofanya ziara mgodini hapo.
Shamika ameeleza kuwa kama wangelikuwa wanatumia Nishati ya Umeme wangeweza kutumia kiasi Cha shilingi Milioni 250 hadi 300 kulipia bili za umeme na kuokoa kiasi Cha zaidi ya shilingi Milioni 700 ambapo Fedha hiyo ingetumika kufanya mambo mengine.
"Matumizi ya Nishati ya Mafuta (Diesel) kwa uendeshaji wa Mtambo wa uchenjuaji kwa siku ni wastani wa Lita 12,000. Mgodi unatumia takribani Lita 3,000 kwa siku kwaajili ya kuendesha Mitambo ya uchimbaji na ubebaji mbale (ore) na miamba bure (waste). Alieleza Mhandis Gilay.
Ameongeza kuwa licha ya kufanya vizuri Mgodi huo unakabiriwa na changamoto mbalimbali ikiwemo Ukubwa wa Deni walilorithi la zaidi ya shilingi Bilioni 42, Ufinyu wa mtaji, Uchakavu wa Miundombinu pamoja na wizi wa Mchanga.
Kwaupande wake Mhandisi Ezra Chiwelesa ameushukuru uongozi wa Mgodi huo kwa namna wanavyoweza kuendesha vizuri na kuwapelekea kupata hati Safi licha ya kukabiliwa na changamoto lukuki.
Chiwelesa ameiomba wizara ya Nishati kushirikiana na wizara ya Madini kuingilia Kati kero ya Umeme katika mgodi huo Ili kuweza kusaidia mgodi huo kuacha kujiendesha kwa hasara kutokana na kukosekana kwa umeme.
"Hapa mnapata hasara kubwa Sana hasara ambayo inaweza kuzuilika, nimepita hapo nje nimeona umeme umefika hadi geitini nashangaa kwanini hamjaanza kuutumia?" Alihoji Mbunge Chiwelesa.
Ameongeza kuwa kwa mujibu wa maelezo ya wataalamu wa umeme mgodini hapo ni kwamba umeme uliofikishwa hapo ni mkubwa kulingana na matumizi ya ndani ya mgodi na kuongeza kuwa kinachotakiwa ni tanesco kujenga kituo Cha kupozea umeme (substation) Ili kupatikana umeme unaotakiwa kutumika ndani ya mgodi na hilo ndilo jambo lililokwamisha hadi sasa.
Sambamba na hayo Mbunge huyo ameuomba uongozi wa mgodi kuwapa Maeneo yenye Madini wananchi ( wachimbaji wadogo wadogo) wanaozunguka Mgodi huo Ili kuweza kuchimba na kuweza kujipunguzia ukali wa maisha pamoja na kuweka uhusiano mzuri baina ya kijiji na Mgodi.
Mbunge wa Jimbo la Bihramulo Mhandisi Ezra Chiwelesa aliyesimama akiongea na uongozi wa mgodi wa Stamigold uliopo wilayani Biharamulo kuhusu namna wanavyojiendesha.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇