BARAZA la Sanaa la Taifa (BASATA) kushirikiana na
vikundi viwili vya sanaa wameandaa tamasha la wanafunzi 250 kutoka shule
tano za msingi litakalofanyika Alhamisi ya Mei 20 kwenye ukumbi wa
BASATA, Dar es Salaam.
Mratibu
wa tamasha hilo, Ramadhani Maneno (Pendapenda) alisema lengo la Tamasha
hilo ni kukuza utamaduni wa mtanzania kwa watoto ujumbe ukiwa ni kupiga
vita umasikini dhidi ya korona.
Pendapenda
ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kikundi cha Sanaa cha Safi Theatre
kitakachoshiriki tamasha hilo alizitaja shule zitazoshiriki tamasha hilo
ni Blessed Hill ya Kitunda, Shule ya Msingi Umoja ya Ilala na Shule ya
viziwi ya St. Augustino ya Buguruni.
Mratibu
hiyo alisema kikundi kingine ni shule ya msingi ya Joyfull kutoka
Bagamoyo mkoa wa Pwani na mgeni rasmi ni Diwani wa Kata ya Buguruni,
ambaye pia ni Katibu wa Madiwani wa Wilaya ya Ilala, Busoro Pazi.
Alisema
tamasha hilo pia litasidizwa na vikundi maarufu vya sanaa vya Safari
Theatre, Hisia Theatre, Happy Centre, Baba Watoto, Tatanisha Dance Crew,
Butterfly Lion Group, Kibasila Sanaa Group vyote vya Dar es Salaam.
Pendapenda alisema zawadi mbalimbali zitatolewa kwenye tamasha hilo za ngao na kila kikundi kitakachoshiriki vitapewa cheti.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇