***********************
NA FADHILA KIZIGO
Kuelekea kwenye derby kubwa Tanzania na Afrika mashariki kati ya Simba na Yanga ni mchezo unaobeba hisia kubwa kwa mashabiki na wadau wa soka nchini hivyo ni mchezo usiotabilika kwa kuangalia rekodi ya nyuma ya derby hizi na hata kwa ubora wa vilabu hivi kwa wakati husika ila unaweza kuangalia zaidi ubora wa mbinu za makocha wawili kati ya Nabi na Gomezi na kupata taswira nzima ya mchezo .
TACTICAL
KOCHA NABI, sitarajii kumuona akifunguka zaidi dhidi ya Simba isipokuwa atacheza kimkakati zaidi kulingana na aina ya wachezaji wake kwa kuzingatia haya .
Individual Tactically ,kwa kutumia mchezaji mmoja mmoja kocha Nabi analo jukumu la kuwatumia wachezaji wake kimkakati zaidi ili kufikia lengo la mchezo husika .
Group Tactical ,Kupitia maeneo matatu kwa maana ya defence line , midfielder na striker kuwe na uongozi maalum wa kila mmoja kutekeleza majukum yake kwa wakati sahihi na kwa dk zote za mchezo .
Team Tactical ,kucheza kinidhamu kwa kuzingatia kanuni ya mchezo kama wakipoteza mpira wafanye jukumu la kujilinda na wakiwa na mpira washambulie .
KOCHA GOMEZ, kwa muendelezo wa matokeo mazuri ya kocha Gomez unaweza sema yeye ndio anaenda kuchukua alama tatu dhidi ya mpinzani wake lakini tusisahau kuwa hii ni derby na kila mmoja anaweza kubadilika na kinaweza kutokea chochote ambacho hatukutarajia na hii ndio derby inavyokuwa kwa aina ya kikosi cha Simba kilivyo kwa sasa naona Simba ikifanikiwa kwenye maeneo haya.
Individual performance,Simba ina aina ya wachezaji wenye uwezo mkubwa wa kucheza derby nyingi na wana uzoefu mkubwa wa kucheza mechi za ushindani zaidi hivyo kupitia aina ya wachezaji wake kama Mickson,John Boko ,Medie Kagere ,Clotus Chama na upana wa kikosi chao naona kocha Didier Gomez akifanikiwa kupitia wachezaji wake .
Schologicaly , kutokana na matokeo mazuri ya Simba kwenye ligi kuu,na klabu bingwa Afrika yanawaweka kwenye hatua nzuri kuelekea kwenye derby dhidi ya wapinzani wao hivyo kiakili Simba wapo sawa kukabiriana na mtani wake pengine unaweza kudharau hili ila ni moja ya ushindi wa Simba kuelekea kwenye mechi hii na kufanikiwa kwa kocha Didier Gomez kunatokana na hili .
Game plan , Kocha Gomez ni mzuri wa game plan kulingana na uhitaji wa mechi kwani tumeliona hili kwenye klabu bingwa na kuwavusha kwenye hatua nyingine hivyo kwenye hili Gomez tunataraji mbinu zaidi kutumika .
SIMBA AU YANGA
Ni mchezo ambao utaamuliwa kwa ubora wa mbinu kati ya makocha wawili wenye historia ya kufundisha klabu moja kila mmoja kwa wakati wake El Mereck ya Sudan hivyo tunataraji kuvimbiana zaidi uwanjani yaani namaanisha kimbinu zaidi hivyo yeyote anaweza kupata alama tatu muhimu kwenye mchezo muhimu ambao Tanzania yote na wapenda soka wakisubiri kwa hamu kubwa mchezo huu , kazi kwenu Nabi na Didier Gomez
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇