LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

May 23, 2021

RAIS SAMIA ATEUA MABALOZI 23, MISS TANZANIA 1999 HOYCE TEMU NDANI

Dar es Salaam
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa mabalozi 23 akiwemo Mrembo wa Tanzania mwaka 1999, Hoyce Temu (Pichani), ambaye kwa sasa ni 
Mwandishi wa Habari na Mjasiriamali.

Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa wamo Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ) Luteni Jenerali Yakub Mohamed na Mkuu wa Kamandi ya Wanamaji JWTZ Meja Jenerali Richard Makanzo.


Pia Rais amemteua Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa zamani Pereira Ame Silima ambaye pia ni Naibu Waziri Mstaafu wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Msaidizi wa Rais Diplomasia, Ofisi ya Rais Ikulu Maulidah Hassan.


Rais amewateua pia Msaidizi wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, Togolani Edriss Mavura na  Edwin Novath Rutegaruka ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE).


Wengine ni Fredrick Ibrahim Kibuta ambaye ni Afisa Mwandamizi katika Ofisi ya Rais, Ikulu, Noel Emmanuel Kaganda Afisa Medani, Ofisi ya Rais, Ikulu na Mindi H. Kasiga Mkurugenzi wa Masoko wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB).


Raus amemteua Caroline Kitana Chipeta ambaye ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Sheria, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,  Macocha Moshe Tembele ambaye ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Agnes Richard Kayola ambaye ni Kaimu Mkuu wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Amemteua Bw. Masoud Abdallah Balozi. Bw. Balozi ni Kaimu Mkurugenzi wa Ofisi ya Mambo ya Nje – Zanzibar, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Taarifa hiyo imesema wengine ni Ceasar George Waitara ambaye ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australia, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,. Swahiba Habib Mndeme ambaye ni Afisa Mwandamizi katika Ubalozi wa Tanzania Washington D.C nchini Marekani na Said Juma Mshana ambaye ni Afisa Mwandamizi katika Ofisi ya Rais, Ikulu.

Amewateua pia Alex Gabriel Kallua ambaye ni Afisa Mwandamizi katika Ofisi ya Rais, Ikulu,Mahmoud Thabit Kombo ambaye ni Waziri Mstaafu wa Utalii na Mambo ya Kale, Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale, Zanzibar na James Gillawa Bwana ambaye ni Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa wa Shinyanga.

Wengine ni Said Shaib Mussa ambaye ni Naibu Mkurugenzi, Ofisi ya Rais, Zanzibar, Elsie Sia Kanza ambaye ni Mshauri Maalum wa Rais kwenye Jukwaa la Uchumi Duniani (World Economic Forum) na Robert Kainula Kahendaguza ambaye ni Naibu Balozi, Umoja wa Mataifa, Geneva.

Taarifa hiyo umesema Uteuzi wa Mabalozi hawa umeanza Mei 22, 2021 na wataapishwa kwa tarehe zitakazotangazwa baadaye.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages