LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

May 23, 2021

OFISI YA RC KAGERA KWA KUSHIRIKIANA NA TANLAP YAFANIKIWA KUTOA HUDUMA ZA KISHERIA KWA WANANCHI 261 KYERWA

 Na Lydia Lugakila, Kyerwa

Ofisi ya mkuu wa mkoa wa Kagera kwa kushirikiana na mtandao wa watoa huduma za msaada wa kisheria TANLAP chini ya ufadhili wa shirika la umoja wa mataifa linalohusika na wanawake (UNWOMEN) wamefanikiwa kutoa huduma ya kisheria kwa wananchi 261 katika wilaya ya Kyerwa mkoani Kagera huku kesi 120 zikipatiwa ufumbuzi.


Akizunguza katika kilele cha maadhimisho ya huduma ya utoaji msaada wa kisheria  mkurugenzi mtendaji TANLAP Bi Christina Kamili amesema kuwa wamefanikiwa pakubwa katika utoaji wa huduma ya msaada wa kisheria katika kata 2 za Mabira na Nkwenda kwa kutoa msaada huo kwa wananchi wapatao 261 katika wilaya hiyo.


Bi Christina amesema kuwa kesi nyingi zilikuwa katika dawati la vitambulisho vya taifa (NIDA) ambapo jumla ya kesi 120 zilikuwa zinahitaji msaada kutoka dawati hilo huku kesi nyingi zikiwa za migogoro ya ardhi, ukatili wa kijinsia ambapo katika kata ya mabira imepatikana kesi ya kupigwa kwa mwanamke mmoja kesi ambayo imepekwa polisi na kuongeza kuwa kwa mwaka 2020 zilipatikana kesi 500 kwa wilaya 3 ambazo ni Kyerwa, Karagwe na Biharamulo na kuwa elimu iliyotolewa ni ya kutosha ambapo tayari kwa sasa wanachi wa wilaya hiyo wametengenezewa nyaraka za kupeleka mahakamani na baraza la ardhi hivyo kuzihimiza taasisi zinazotoa huduma za msaada wa kisheria kikiwemo  chama cha mawakili na Mhora kuendelea kutoa huduma ya msaada wa kisheria kwa wananchi.


Kwa upande wake afisa mwandamizi upatikanaji haki,  kutoka shirika la Un women Bi, Rachael Boma amewahimiza wananchi wilayani humo kujenga mazoea ya kujitokeza kupata msaada wa kisheria inapobidi katika maeneo yao, huku akimshukuru mkuu wa wilaya hiyo pamoja na watendaji wake, wananchi kwa ushirikiano katika huduma hiyo na kuahidi kuendelea kutoa kushirikiana na serikali pamoja na wadau mbali mbali.


Akihitimisha kongamano la wiki ya kisheria lililofanyika kwa siku 2 wilayani Kyerwa katika kata za Mabira na Nkwenda mkuu wa wilaya hiyo Rashid Mohamed Mwaimu awamewapongeza wadau mbali mbali kwa uandaaji wa kongamano hilo na kuziomba taasisi zote zilizohusika katika kutoa huduma ya msaada wa kisheria kwa wananchi kuhakikisha kero ambazo hazijapatiwa ufumbuzi kuendelea kutatuliwa.


Mwaimu amesema wilaya hiyo imeendelea kugubikwa na vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa watoto yatima, wajane, wanaume pia migogoro ya ardhi kukemea vitendo hivyo na kuwataka wananchi kutoa taarifa katika vyombo husika vya kisheria.


Aidha kwa upande wake msajili msaidizi wa watoa huduma za msaada wa kisheria mkoani Kagera Issa Malimi ameipongeza Ofisi ya mkuu wa mkoa huo kwa maadalizi ya huduma hiyo na kuwaomba wananchi mkoani humo kutovifumbia macho vitendo vyote ya kiukatili badala yake watumie taasisi husika kumaliza kero zao


"nawapongezeni TANLAP na Un women pamoja na wadau wengine kwa kufanikisha shughuli hii kwani katika wilaya yangu yalikuwepo matukio ya ndani ambayo hayakuweza kutatuliwa kwa wakati lakini naamini kupitia elimu mlioitoa naamini itawanufaisha wananchi wangu"alisema mkuu wa wilaya hiyo.


 Kilele cha maadhimisho ya huduma ya utoaji msaada wa kisheria  yamehusisha taasisi mbali mbali za utoaji msaada wa kisheria ikiwa ni pamoja  Mamlaka ya vitambulisho vya taifa( NIDA), taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) MHORA, MAHAKAMA, USTAWI WA JAMII, IDARA YA ARDHI, DAWATI LA JINSIA IDARA YA UHAMIAJI na kubeba kauli mbiu  isemayo "mwanamke inuka omba msaada wa kisheria kwa ustawi wa maendeleo yako"

Bi Rachael Boma akitoa shukrani kwa wadau mbali mbali waliofanikisha maadhimisho hayo

Bi Christina Kamili akihutubia katika kilele cha maadhimisho ya huduma ya msaada wa kisheria
Sehemu ya wananchi walionufaika na huduma ya msaada wa kisheria
Mkuu wa wilaya ya Kyerwa mkoani Kagera Rashid Mohamed Mwaimu akizungumza na wananchi hao

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages