Mbunge wa Jimbo la Nachingwea Mkoani Lindi Amandus Chinguile amekabidhi mifuko ya saruji 1,800
Mei 22 /2021 ikiwa ni Moja ya ahadi yake katika sekta ya ELIMU aliyoitoa wakati akiomba ridhaa katika uchaguzi Mkuu 2020.
Vifaa hivyo vimekabidhiwa katika kata 16 kwa lengo la kuboresha miundombinu ya shule za sekondari ndani ya kata hizo.
Akizungumza
mara baada ya kukabidhi vifaa hivyo,Mbunge wa Jimbo la Nachingwea
Amandus Chinguile alisema 'yeye kama Mbunge anao wajibu wa kuhakikisha
wanafunzi wanasoma katika mazingira rafiki kwa kuwaboreshea miundombinu.
Alisema kuwa ataendelea kuziangazia shule zenye changamoto na kuziwekea mazingira rafiki ya kujifunzia.
Vifaa hivyo vinatarajia kutumika kakamilisha ujenzi wa vyumba vya madarasa 22 katika Shule za Sekondari zilizopo Jimboni humo.
"Ni
wajibu wetu sisi kama viongozi na wadau mbalimbali kuhakikisha
tunashirikiana kwa pamoja kuinua Elimu katika wilaya yetu kwa
kuhakikisha tunaiboresha Miundombinu ya shule"Alisema Chinguile.
Aliongeza
kuwa, hii awamu ya kwanza ameziangazia kata 16 katika sekta ya
Elimu,akini ataendelea kutatua changamoto zinazowakabili wananchi katika
kata nyingine.
'Ili Jimbo liendelee kupiga hatua
kimaendeleo nitaendelea kutatua kero zinazowakabili wananchi kwa
kuimarisha miradi ya Maendeleo katika sekta ya Maji,Afya ikiwemo
kuisimamia Serikali katika sekta ya Kulimo ili pembejeo za Kilimo ziweze
kuwafikia kwa wakati na zipatikane kwa bei nafuu.
Safi saana mbunge wetu kwa juhudi unazozifanya
ReplyDelete