MBUNGE wa Viti Maalumu (CCM) kupitia Asasi za Kiraia Tanzania Bara (NGOs) Neema Lugangira akiwa Bungeni Jijini Dodoma leo |
Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe Profesa Kitila akijibu hoja mbalimbali
NA MWANDISHI WETU, DODOMA.
MBUNGE wa Viti
Maalumu (CCM) kupitia Asasi za Kiraia Tanzania Bara (NGOs) Neema
Lugangira ameitaka Wizara ya Viwanda na Biashara itoe Kanuni za Food
Labelling zitakazowalinda walaji na sio kuendelea kuweka maisha ya
Watanzania rehani.
Ameyasema hayo leo
Bungeni Jijini Dodoma wakati akichangia Bajeti ya Wizara ya Viwanda na
Biashara kupitia Mchango wa Maandishi na Taarifa aliyotoa ambapo alisema
hilo linatokana na hivi sasa kuwepo kwa changamoto ya Usalama wa
Chakula yaani Food Safety unaochangiwa na baadhi ya majukumu ya TFDA ya
kupelekwa Shirika la Viwango Tanzania (TBS).
Akichangia kupitia
Mchango wake wa Maandishi Mbunge Neema Lugangira alianza kwa kuikumbusha
Wizara ya Viwanda na Biashara kuwa moja ya majukumu yake ni kufuatilia
na kutathimini utendaji katika viwanda, biashara, masoko, viwanda vidogo
vidogo na biashara ndogo ndogo ikiwemo taasisi zinazowezesha maendeleo
viwanda na biashara.
Alisema sanjari na
jukumu hilo baada ya Marekebisho ya Sheria ya Viwango ya Mwaka 2009
iliyochukua majukumu ya TFDA na kuyahamishia TBS ikiwemo jukumu la
kusimamia Ubora na Usalama wa Chakula .
Aidha alisema Wizara
ya Viwanda na Biashara imefanya kazi kubwa ya kuhamasisha uwekezaji
kwenye viwanda vya kuchakata na kusindika vyakula nchini na inastahili
pongezi kubwa lakini kuna changamoto katika eneo la Usalama wa Vyakula
nchini.
“Nasema hivi kwa
sababu nyanya inaweza kupuliziwa dawa siku kama ya jana na ikavunwa leo
leo au kesho nyanya hiyo ikiuzwa sokoni mwananchi akainunua na
kutengeneza kachumbari na akala jambo ambalo linaweka hatarini maisha
yake kutokana na chemikali hatari zilizopo kwenye nyanya” Alisema
Mbunge Neema
Lugangira aliongeza kuwa wakati mwengine wananunua juisi ya box kama ya
juisi ya chungwa wakiamini juisi ile ni ya chungwa halisi lakini mara
nyingi kinachokuwepo ndani ni Concentrate, rangi, ladha na sio chungwa
halisi pia kiwango cha sukari kinachokuwepo ni hatari sana.
“Huu ni mfano ambao
unaweza kupelekea udanganyifu mkubwa unaochangia kwa kasi ongezeko la
tatizo la uzito uliozidi na viribatumbo nchini hususan kwa watoto wadogo
ambao ni wanywaji wakubwa wa juisi ni za box.
Katika mfano mwingine
Mbunge Lugangura alisema wananchi tunanunua Yoghut ya Strawberry
tukiamini ndani kuna Strawberry halisi jambo ambalo mara nyingi sio
kweli bali kinachokuwepo ni rangi na ladha japo kwenye kopo la
Yoghurt/Mtindi inakuwepo picha ya tunda la Stawberry.” Alisema
Mbunge alisema hali
hiyo ipo hata kwenye bidhaa za vyakula zingine ikiwemo mafuta ya
kupikia, ice cream ambapo changamoto hiyo inawezeshwa kwa kiasi kubwa na
Mfumo wa sasa wa kuweka lable/lebo kwenye Vifungashio vya Chakula yaani
Food Labelling; jambo ambalo linaweza kuhatarisha Maisha ya Watanzania
kwa sababu hivi sasa wengi wetu tunanua bidhaa za vyakula pasipo kuelewa
nini haswa kimo ndani yake hivyo hatujui usalama wake.
Aliongeza kuwa Wizara
ya Viwanda na Biashara inalo jukumu la moja kwa moja la kuimarisha
Usalama wa Vyakula vinavyochakatwa na kusindikwa na viwanda na biashara
zilizochini ya Wizara na kutokufanya kitu na kuendelea kuweka Maisha ya
Watanzania Rehani.
“Kwa mantiki hiyo
ningependa kukushauri wewe kama Waziri wa Viwanda na Biashara uandae
Kanuni za Food Labelling zitakazoweka ulazima wa wachakataji na
wasindikaji wa vyakula kuandika wazi kilichopo ndani na takwa hilo liwe
kwa bidhaa za vyakula zinazozalishwa nchini na zinazotoka nje ya nchi”
Alisema Mbunge Lugangira
Hata hivyo alisema
kama wameweza kufanya hivyo kwa Sigara ambazo juu yake pakiti inasema
wazi uvutaji wa sigara ni hatari kwa maisha yako kwanini wasindwe kwenye
bidhaa za vyakula?
Mbunge Neema
alisisitiza pia umuhimu wa Wizara kuanzisha Kampeni ya Elimu kwa Umma ya
kuwaelimisha jamii maana ya Food Labelling watakazopendekeza kupitia
Kanuni ili kila Mtanzania aweze kufanya maamuzi sahihi kutokana na
manunuzi ya chakula jambo ambalo hata Chama cha Mapinduzi imegusia
kupitia Ilani ya Uchaguzi ya CCM mwaka 2020-2025 Ibara ya 49(7) ukurasa
wa 61 kwa kusema “
CCM itaelekeza Serikali kubuni na kuendeleza mikakati
ya uhamasishaji wa Watanzania kupenda kutumia bidhaa zinazozakishwa
katika viwanda vya ndani” na hii lazima iende sanjari na kumlinda mlaji
atakae nunua bidhaa za vyakula.
Mbunge Neema
Lugangira alimalizia kwa kusema ni matarajio yake Wizara ya Viwanda na
Biashara itafanyia kazi ushauri wake na Tanzania inaweza kujifunza toke
nchi zingine kama Chile.
Wakati wa kuhitimisha
Hoja yake ya Bajeti, Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe Profesa Kitila
Mkumbo aligusia Ushauri aliotoa Mbunge Lugangira wa kuandaa Kanuni za
#FoodLabelling na kuahidi kuliangalia na kuondoa mapungufu yaliyopo.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇