Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako, Naibu Waziri wa wizara hiyo, Omar Kipanga wakikagua maendeleo ya ujenzi wa shule ya mfano ya Iyumbu jijini Dodoma leo. |
Askari wa Suma Jkt wakiendelea na ujenzi wa nyumba za walimu.
Waziri Profesa Ndalichako akikagua ujenzi wa nyumba za walimu.
Naibu Waziri Kipanga akipima ubora wa ujenzi kati ya nguzo na nguzo.
Ujenzi ukiendelea
Msimamizi Mkuu wa Mradi huo, Meja Philimon Komanya akielezea kuhusu maendeleo ya ujenzi wa mradi huo na kwamba kwa sasa umefikia aslimia 27.
Waziri Ndalichako akizungumza na vyombo vya habari baada ya kumaliza kukagua ujenzi huo. Kushoto ni Naibu Waziri Kipanga na Msimamizi Mkuu wa Mradi huo, Meja Komanya.
WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako amelitaka Shirika la Suma JKT linalojenga Shule ya Mfano ya Iyumbu jijini Dodoma, kukamilisha ujenzi wa shule hiyo mapema Januari 2021 ili shule hiyo ianze kutumika.
Waziri Ndalichako ambaye ameambatana na Naibu Waziri Omar Kipanga ametoa agizo hilo wakati wa ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa shule hiyo ambayo kimkataba ujenzi wake unatakiwa kukamilika Februari mwakani.
Aidha, Profesa Ndalichako amewaagiza Suma JKT kujenga mradi huo kwa ubora unaoendana na michoro ya mradi ilivyo.
Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza kupitia kwenye clip hii ya video, Waziri Ndalichako na Msimamizi Mkuu wa Mradi kutoka Suma JKT, Meja Philimon Komanya wakielezea jinsi shule hiyo itakavyokuwa na mambo mengi muhimu na ya kipekee nchini....
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇