LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Apr 10, 2021

MBUNGE NEEMA LUGANGIRA AIBUA MJADALA MAMILIONI KUTUMIKA KILA MWEZI KULISHA CHAKULA MAHABUSU

 

MBUNGE wa Viti Maalumu CCM kupitia Kundi la Asasi za Kiraia (NGOs) Mhe Neema Lugangira akizungumza wakati akichangia mchango wake Bungeni Jijini Dodoma wa kuboresha Mpango wa
Maendeleo ya Taifa uliojikita kuishauri Serikali kupunguza gharama kubwa ya kuwalisha chakula mahabusu ili fedha zitakazookolewa zielekezwe  kwenye utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo.
 

MBUNGE wa Viti Maalumu CCM kupitia Kundi la Asasi za Kiraia (NGOs); Mhe Neema Lugangira ameibua mjadala mpya kuhusu mamilioni ya fedha ambazo zimekuwa zikitumika kila mwezi kulisha chakula mahabusu hapa nchini baada ya
kuishauri Serikali ichukue maamuzi madhubuti ya kuona namna ya kupunguza idadi ya mahabusu waliopo magerezani ili kupunguza gharama hizo
zinazotumika.

Mbunge Neema ameibua mjadala huo wakati akichangia
mchango wake Bungeni Jijini Dodoma wa kuboresha Mpango wa Maendeleo ya Taifa uliojikita kuishauri Serikali kupunguza gharama kubwa ya kuwalisha chakula mahabusu ili fedha zitakazookolewa zielekezwe kwenye
utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo.

Alisema iwapo idadi hiyo ikipunguzwa itasaidia kuokoa fedha ambazo hivi sasa Jeshi la Magereza linatumia Milioni 900 kila mwezi  kwa aili ya chakula cha Wafungwa na Mahabusu zitasaidia katika masuala mengine mbalimbali ya kimaendeleo
hapa nchini.

Mbunge Neema alisema alisema anaamini kwamba
wanapozungumzia kuchangia kuboresha Mpango wa Maendeleo ya Taifa ni lazima pia waangalia namna ya kupunguza mzigo usiokuwa na lazima kwa
Serikali na ili Fedha zitakazookolewa ziekelezwe eneo jingine ambalo linastahili kwa sababu yeye binafsi anaona huo ni upotevu wa Fedha ambazo sio za lazima.

“Pamoja na ushauri huu Mh Naibu Spika
nashauri njia nyengine ambazo Serikali inaweza kufanya ni Mahakama ibebe
jukumu la kugharamia Bajeti ya kulisha mahabusu waliopo gerezani kwa
sababu kimsingi wapo huko kutokana na ucheleweshwaji wa ucheleweshwaji
wa kesi zao kupata
hukumu” Alisema Mbunge Neema

Aidha, Mhe Neema Lugangira aliongeza kwamba hata Jeshi la Polisi pia pengine linajukumu kwenye hili kwa sababu bila kufanya hivyo ni kuendelea kulionea Jeshi la Magereza wakati Serikali imesema lijitegemee wakati halina vyanzo mapato hivyo ni matumaini yake kwamba wakati Waziri wa
Fedha na Mipango, Mhe Mwigulu Nchemba atakapo wasilisha muelekeo kulingana na maoni mengi yaliyotolewa atazingatia ushauri wake maana jambo hili analijua vizuri sana ukizingita alikuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Waziri wa Katiba na Sheria.

“Kwani ni lazima Serikali ifika mahali iangalie suala la idadi kubwa ya mahabusu waliopo gerezani na nasema hivyo kwa sababu hivi sasa Tanzania ina wafungwa takribani 16,836 na mahabusu 16,703 ambapo Jeshi la Magereza kila mwezi inatumia milioni 900 kwa ajili ya kuwalisha wafungwa na mahabusu hiyo ni gharama kubwa
sana kwa serikali” Alisema Mbunge Neema

“Sasa tupate picha kidogo ikiwa tutaweza kupunguza idadi kubwa ya mahabusu gezerani inamaana kati
ya hiyo milioni 900 kila mwezi inayotumika na Jeshi la Magereza kwa ajili ya  kulisha chakula wafungwa na mahabusu tukiweza kupunguza idadi ya hao mahabusu ina maana kuna kiasi kikubwa cha fedha kinaweza
kuokolewa na kiasi hicho iila mwezi kitakwenda kufidia kiasi kikubwa cha fedha ambacho kinahitajika ili kutekeleza mipango mbalimbali na ushauri uliotolewa na wabunge” Alisema Mbunge Neema Lugangira.

Mhe Neema Lugangira alikumbushia pia Hotuba za hivi karibu za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Rais Samia Suluhu Hassanaliliongelea suala la idadi kubwa ya mahabusu kwenye magereza hivyo ni matarajio yake jambo hili litapewa uzito unaostahili.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages