LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Apr 18, 2021

UMISHI WATAKIWA KUSIMAMIA UTEKELEZAJI AHADI ZA MASUALA YA KIUTUMISHI NA UTAWALA BORA ZILIZOAINISHWA KWENYE ILANI YA CCM

Na James  Mwanamyoto, Utumishi

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Deogratius Ndejembi, amewataka Watumishi wa Ofisi yake kusimamia utekelezaji wa ahadi za masuala ya kiutumishi na utawala bora zilizoainishwa kwenye Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ya Mwaka 2020 ili kuhakikisha Sekta ya Umma inaimarika na kutoa huduma bora kwa wananchi. 


Ndejembi ametoa mwito huo wakati akifungua Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, uliofanyika, leo jijini Dodoma. Ndejembi amefungua kikao hicho kwa niaba ya Waziri wa Wizara hiyo Mohamed Mchengerwa


Amelitaka baraza hilo kupitia na kuchambua Ilani kwa kina na kubaini ahadi zinazohusu Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa lengo la kuhakikisha utekelezaji wake unafanyika kwa ufanisi mkubwa ili kuboresha utoaji huduma kwa wananchi.


Akihimiza utekelezaji wa Ilani katika Taasisi za Umma, Ndejembi amewataka Watumishi wa Umma kuendelea kuchapa kazi kwa bidii na weledi ili kuiwezesha Serikali kutekeleza ahadi ya kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.


Ndejembi amesema, licha ya Watumishi wa Ofisi ya Rais-Utumishi kufanya kazi kwa weledi katika kutekeleza Ilani, lakini wana jukumu kubwa la kuhakikisha wanabadili mtazamo hasi dhidi yao kwani malalamiko mengi yanayowasilishwa Utumishi yanatokana uzembe wa Watumishi wa Taasisi nyingine.


Akitoa neno la shukrani kwa niaba ya wajumbe wa baraza, Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji Sera, Agnes Meena amemuahidi Mhe. Ndejembi kuwa, Utumishi itahakikisha inaishauri vizuri Serikali kutekeleza Ilani na kuongeza kuwa, watumishi wataendelea kufanya kazi kwa bidii na weledi ili kuiwezesha ofisi kufikia malengo yake.


Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora imefanya kikao cha Baraza la Wafanyakazi kwa mujibu wa sheria, ambapo Taasisi za Umma zinapaswa kukutana kupitia mpango na bajeti itakayowasilishwa Bungeni, kabla Bunge la halijapitisha bajeti husika kwa ajili ya utekelezaji.


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Deogratius Ndejembi akifungua kikao cha Baraza la Wafanyakazi Ofisi ya Rais-UTUMISHI kwa niaba ya Waziri wa Wizara hiyo Mohamed Mchengerwa.
Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji Sera, Agnes Meena akitoa neno la shukrani kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Deogratius Ndejembi kwa niaba ya wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Rais-UTUMISHI mara baada ya Naibu Waziri huyo kufungua kikao cha baraza hilo.
Baadhi ya Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi Ofisi ya Rais-UTUMISHI wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya ais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi wakati akifungua kikao cha Baraza hilo kwa niaba ya Waziri Mchengerwa.
N
aibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,  Deogratius Ndejembi akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Rais-UTUMISHI, baada kufungua kikao cha baraza hilo kwa niaba ya Waziri Mchengerwa

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages