Mchungaji Maliga wa kanisa la EAGT Nkuhungu East akiubiri Injili
Moja ya kwaya ambayo ilihudumu katika ibada ya jumapili ya Pasaka
Na Kadala Komba, Dodoma
Mchungaji John Maliga wa kanisa la EAGT Evalingelist Assembles of God lililopo Nkuhungu jijini Dodoma amewataka watu kujitathimini Matendo yao katika ya kipindi hiki Cha Pasaka sio kutenda dhambi,kwani hiki ni kipindi Cha kutenda Matendo Mema kujitoa kwa ajili ya watu wengine Kama alivyofanya Yesu kwa ajili ya wanadamu.
Mchungaji John alisema ngoja nikupe Siri moja mpendwa huwenda ulikuwa huijui Yesu amekubali kufa msalabani kifo Cha aibu ili Mimi na wewe tuokolewe, Yesu alikuwa hana Dhambi yoyote alitulia Mbinguni kwa Baba yake, alikubali kuacha kila kitu Mbinguni akaja kwetu sisi ili kutukombo kututoa katika Giza na kutuweka katika mwanga mkuu Soma Biblia yako Mathayo Mtakatifu sura ya 24:1:12 Alisema.
Mchungaji Maliga aliyasema hayo jumapili ya Pasaka alipokuwa akiubiri Injili kanisani hapo na kusisitiza kwamba Neno la Mungu ni mkate wa uzima, mpendwa unapoingia nyumbani mwa Bwana utatoka Kama ulivyo ingia usiingie kanisani kwa mazoea Soma Mathayo Mtakatifu 28:1:15 Hii ndiyo Pasaka ya kweli Alisema mchungaji Maliga.
Sambamba na hilo Mchungaji Maliga alisema Sisi Tulio okoka tuna Jukumu moja tu la kuombea Taifa kumwombea Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan katika utekelezaji wa majukumu ya kuijenga nchi yetu ya Tanzania Alisema mchungaji Maliga .
Pia mchungaji Maliga amewasii waumini wake Kukaa kimya pindi wanapokutana na matatizo alisema sio kila kitu unachosemeshwa unatakiwa kukijibu hapana jifunze kunyamaza maana unaweza kujibu ukajikuta unakosea ukaingia kwenye matatizo mazito, kunawatu wanataka kuona wewe unapata matatizo kila siku hawapendi kukuona una Furaha Tujifunze kwa Yesu Luka Mtakatifu 23:1:25 Alisema mchungaji Maliga.
Aidha Mchungaji Maliga aliwakumbusha waumini kuwa makini na Marafiki ambao wapo nao siku zote utasema mchungaji anamaanisha nini? Ni hivi ukiwa na kitu ambacho kwa Marafiki zako ni msaada kwao utakuwa na Marafiki wengi Sana Ila kumbuka hawapo kwajili yako wapo kwajili ya icho kitu ulichonacho kitu ulichokibeba, Kama haunakitu kamwe uwezi kuwa na Marafiki wengi kwa sababu kwa wakati uwo uwezi kuwafaa kwa chochote, Mpendwa wangu Tafuta kuwa Rafiki wa Yesu Yeye awezi kukuacha pindi hauna kitu Tena upendo wake haupimiki hata kwa mizani Alisema.
Mwisho Mchungaji Maliga alisema kunawatu leo wanakesha kanisani wanamwomba Mungu awape ajira,awape watoto awapandishe vyeo awainue kiuchumi lakini Mungu akisha wapatia wanavyo viitaji Basi wanaacha hata kuenda kanisani hata kushukuru pia wanasahau wanaanza kuzitegemea akili zao wenyewe, unajidanganya Mwanangu Kama ulikuwa na akili zako kwanini ulikuwa unakesha kanisani ukiomba aliwauliza washirika? Omba Toba haraka kabda Mungu ajachukua vilivyo vyake mrudie Mungu Yeye anamaarifa, kanuni namna ya kuviendesha vitu alivyokupa, Nawatakia Pasaka njema nendeni na Amani ya Bwana Alisema mchungaji Maliga.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇