Mbunge wa Jimbo la Temeke, Dorothy Kilave akizungumza jambo na baadhi ya Viongozi wa Benki ya CRDB ambapo Kikao hicho kilifanyika muda wa Saa 4:30 Asubuhi Maeneo ya Ofisi ya Mbunge wa Jimbo hilo.
Lengo lakikao hicho ni kufanya Mazungumzo na Benki ya CRDB juu ya kutoa Mikopo ya Riba Nafuu Pamoja na Elimu ya Usimamizi wa Fedha kwa Wananchi wa Jimbo la lake.
Mbunge wa Jimbo la Temeke Mhe Dorothy Kilave George amewaeleza Maafisa hao juu ya namna serikali inavyotoa Mikopo kupitia Manispaa zetu lakini amedhamiria kupanua wigo wa Mikopo katika makundi matatu (Walemavu,Kinamama na Vijana)
Endrew Augustine ambaye ni Manager wa Tawi la CRDB Temeke Amekubaliana na Maombi ya Mhe. Mbunge wa Jimbo la Temeke na ameahidi kuandaa utaratibu maalumu kwa ajili ya kuwanufaisha wananchi wa Temeke kwa Mikopo ya Riba nafuu Pia watashiriki kwa ukaribu sana kuhakikisha wanatoa mafunzo ya usimamizi wa fedha kwa Vikundi na wajasiriamali Kama ilivyokubaliwa.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇