Na Richard Mwaikenda, Dodoma
Mbunge wa YAHAYA OMARI MASARE wa Jimbo la Manyoni Magharibi amepambana bungeni kuhakikisha serikali inakubali kujenga malambo kwa ajili ya wafugaji kunywesha mifugo yao maji.kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Itigi. Masare amehoji bungeni kuwa ni lini serikali itajenga malambo hayo ambapo Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Mdaki alikuwa na majibu yafuatayo; :- Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Mhe. Yahaya Omari Masare – (Manyoni Magharibi ) kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, Wizara kwa kushirikiana na wadau mbalimbali, inategemea ifikapo 2025, itaongeza idadi ya malambo na mabwawa ya maji ya mifugo kutoka 1,384 hadi 1,842 na visima virefu kutoka 103 hadi 225. Aidha, katika mwaka wa fedha 2020/2021, Wizara inakamilisha ujenzi wa mabwawa matatu ya Chamakweza (Chalinze), Kimokouwa (Longido) na Narakauo (Simanjiro) pamoja na ujenzi wa visima virefu viwili cha Usolanga, (Iringa D.C) na Mpapa (Manyoni D.C). Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa 2021/2022, Wizara imepanga kutekeleza ujenzi wa mabwawa matano (5) yenye thamani ya shilingi bilioni 1.6 na visima virefu sita (6) vyenye thamani ya shilingi milioni 560 kwa maeneo yenye changamoto ya ukame na uhitaji mkubwa wa maji nchini. Wizara itaangalia uwezekano wa kuingiza Halmashauri ya Itigi katika mpango kutegemeana na Bajeti. Mheshimiwa Spika, nitoe rai kwa Waheshimiwa Wabunge, Madiwani na Wakurugenzi katika halmashauri zetu, ikiwemo Halmashauri ya Itigi, kutenga na kutumia asilimia 15 ya mapato ya ndani yatokanayo na mifugo kujenga miundombinu muhimu kwa mifugo, ikiwa ni pamoja na mabwawa, majosho, malambo, visima, minada n.k. Pia, Waziri amekubali ombi la Mbunge Masare kuambatana naye jimboni kwenda kujionea hali halisi ya changamoto ukosefu wa malambo kwa ajili ya kunyweshea maji mifugo. Mdau nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii ya video, Mbunge Masare akiuliza na Waziri Mdaki akijibu... Imeandaliwa na Richard Mwaikenda Mhariri Blog ya Taifa ya CCM 0754264203 Your Ad Spot
Apr 8, 2021
SERIKALI YAKUBALI OMBI LA MBUNGE MASARE KUJENGA MALAMBO ITIGI+video
Tags
Bunge#
featured#
Share This
About Richard Mwaikenda
featured
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇