LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Apr 3, 2021

RAIS WA ARGENTINA AAMBUKIZWA CORONA

Rais wa Argentina aambukizwa coronaRais Alberto Fernandez wa Argentina amesema kuwa ameambukizwa virusi vya corona ambapo ana alama kadhaa za maradhi hayo ikiwemo homa na maumivi hafifu ya kichwa.

Alberto Fernandez ameandika leo Jumamosi katika ukurasa wake wa Twitter kwamba jana Ijumaa baada ya kupata homa na maumivu hafifu ya kichwa aliamua kufanyiwa vipimo vya corona ambapo alipatikana kuwa na virusi hivyo.

Rais Alberto Fernandez ambaye mapema mwaka huu aliteuliwa na wabunge wa Bolivia kwa ajili ya kugombea tuzo ya amani ya Nobel kutokana na mchango wake katika kuokoa maisha ya rais wao, Evo Morales, alipolazimika kuikimbia nchi hiyo kutokana na mgogoro wa kisiasa, karibuni hivi alimlazimisha waziri wake wa afya ajiuzulu baada ya kufichuliwa kasha ya kuwapa marafiki zake chanjo ya corona kabla ya kuzinduliwa rasmi mpango wa serilali wa kuwachanja raia wa nchi hiyo.

Evo Morales

Chuo cha John Hopkins cha nchini Marekani kilitangaza jana Ijumaa kwamba Waargentina milioni 2.4 wameambukizwa virusi vya corona ambapo 55,945 kati yao wamepoteza maisha kutokana na maradhi hayo angamizi.

Takwimu za Wizara ya Afya ya Argentina zinaonyesha kuwa hadi sasa nchi hiyo imefanikiwa kuwapa chanjo raia wake laki 7.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages