LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Apr 19, 2021

RAIS SAMIA KULIHUTUBIA TAIFA KUPITIA BUNGE ALHAMISI WIKI HII


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kulihutubia Taifa kupitia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania siku ya Alhamisi ya Wiki hii.


Taaifa zimesema, Rais Samia atafanya tukio hilo la kulihutubia Taifa kupitia Bunge jijini Dodoma, siku hiyo ya Alhamisi, Aprili 22, 2021, kuanzia saa 10 jioni.


Kwa mujibu wa utaratibu wa kawaida wa Kikatiba Rais ni sehemu ya Bunge hivyo anaweza kulihutubia Bunge katika wakati wowote pale haja itakapokuwa ipo.


Rais Samia amekuwa Rais baada ya kuapishwa kuchukua nafasi ya Hayati Dk .John Magufuli aliyefariki Dunia, mapema mwezi uliopita kwa ugonjwa wa moyo.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages