LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Apr 23, 2021

RAIS SAMIA ATEUA MWENYEKITI WA PSRS NA WA TACAIDS, LEO


Ikulu, Chamwino.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amemteua Dk. Hedwiga Swai kuwa Mwenyekiti wa Kamisheni ya Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS).


Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu Chamwino jijini Dodoma, leo, imesema, Rais amemteua pia Sophia Elias Kaduma kuwa Mwenyekiti wa Sekretarieti ya Jira katika Utumishi wa Umma (PSRS).


Taarifa imefafanua kuwa Dk. Swai ameteuliwa kushika wadhifa wa kuwa Mwenyekiti wa TACAIDS kwa kipindi cha pili baada ya kipindi cha kwanza kumalizika.


"Uteuzi wa viongozi hao umeanza leo tarehe 23 Aprili, 2021", Kurugenzi ya Nawasiliano ya Rais, Ikulu imemaliza taarifa yake kwa maelezo hayo.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages