Makamu wa Rais Chama cha Wauguzi na Ukunga (TANNA), Ibrahim Mgoo Leo April 6, 2021 ametia Saini katika Kitabu Cha Maombolezo kufutia kifo cha aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Tanzania wa Tanzania, Rais John Pombe Magufuli katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Manyara mara alipo mtembelea kwa ajili ya Maandalizi ya Maadhimisho ya Siku ya Wauguzi Kitaifa inayo tarajiwa kufanyika Mkoani humo Mei 12, 2021 na Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Mama Samia Suluhu Hassan.
Makamu wa Rais wa Chama Mgoo amesema Maandalizi yanaendelea Vizuri na huku akitoa wito kwa Wauguzi kote Nchini na Watanzania kwa Ujumla kumuenzi Hayati Dkt. John Pombe Magufuli kwa Kuchapa kazi kwa Uadilifu Kama ilivyokuwa Falsafa yake ya Hapa Kazi Tu.
Pia anawakaribisha Wauguzi kote Nchini kwaajili ya Kuadhimisha miaka 200 ya tangu kuzaliwa mwasisi wa Taaluma ya Uuguzi Duniani, Bi. Florence Nightingale
Pumzika Kwa Amani Dkt. John Pombe Joseph Magufuli
Akaribie mama wauguzi tudeke. Yan tutadeka pale uwanjani hapatatosha,full kulia mpaka mama atunyamazishe
ReplyDeleteInshaAllah tuombe her, mh Rais awe Nas siku hiyo muhim kwetu..
ReplyDeleteKila la hell katika siku hiyo
ReplyDeleteSuala la ajira za Wauguzi tafadhari linapaswa kupewa kipaumbele katika ajenda zenu
ReplyDelete