Shibuda akizungumza na vyombo vya habari
Wanahabari wakiwa kazini
Na Richard Mwaikenda, Dodoma
Katibu Mkuu wa Baraza la Vyama vya Siasa Tanzania, John Shibuda amewaomba Watanzania kumuenzi aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano, Hayati Dkt. John Magufuli kwa mambo mazuri aliyoyafanya na kumuunga mkono kwa kuchapa kazi Rais mpya Samia Suluhu Hassan.
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dodoma baada ya kusaini kitabu cha maombolezo ya Hayati Dkt Magufuli, Shibuda ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha TADEA, amempongeza Rais wa Awamu ya Sita wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ambapo pamoja na kumwagigia sifa lukuki amewaomba watanzania kumuunga mkono kwa kuchapa kazi ili Taifa lisonge mbele kimaendeleo.
"Rais Samia, ikubalike ujio wako ni Ari Mpya na chachu ya kuzimua kukomboana kifikra sisi kwa sisi-wewe ndiyo Darubini ya kuchanganua na kupambanua tulikotoka, tulipo na tuendako," amesema Shibuda.
Ndugu, nakuomba uendelee kusikiliza clip hii ya video, Shibuda akizungumza wakati wa hitimisho la maombolezo hayo pamoja na kumpongeza Rais Samia...
IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA MHARIRI BLOG YA TAIFA YA CCM
0754264203
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇