LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Apr 18, 2021

RAIS SAMIA NA RAIS DK. MWINYI WAHUDHURIA KONGAMANO LA KUMUOMBEA DUA RAIS WA AWAMU YA TANO HAYATI JOHN MAGUFULI

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiwa  na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Barazala Mapinduzi Dkt Hussein Ali Mwinyi, Makamu wa Rais Dkt Philip Mpango na viongozi wa dini wa madhehebu mbalimbali akishiriki kuomba dua kabla ya kuanza kwa Kongamano la Viongozi wa Dini la Kumuombea na Kuombea Taifa pamoja na kumshukuru Mungu kwa ajili ya Maisha ya aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano Hayati Dkt. John Pombe Magufuli katika Ukumbi wa Chimwaga jijini Dodoma leo Jumapili Aprili 18, 2021.

Sheikh Mkuu na Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeiry Ally akitoa mada waati wa kongamano la kumuombea dua Hayati Magufuli.
Rais wa Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi akihutub
Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki Dkt John Pallangyo (aliyevaa tai) na Mbunge Pangani Znzibar, Haji Amour Haji wakiwa kwenye kongamano hilo la kumuombea dua Hayati Magufuli.
Mbunge wa Viti Maalumu wa Bunge la Tanzania Asha Abdallah Juma (katikati) na Mbunge mwenzie wa Viti Maalumu Saada Mansour Hussein (kulia) wote kutoka Zanzibar wakiungana na viongozi wengine kumuombea dua Hayati Magufuli.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angeline Mabula (kushoto) akiwa miongoni mwa viongozi waliohudhuria kongamano hilo.
Askofu Dkt. Evance Chande (kulia) wa Kanisa la EAGT Nazaret Ipagala Dodoma akiwa miongoni mwa viongozi wa dini waliohudhuria kongamano hilo la kumuombea Hayati Magufuli.


Wananchi wakiungana na viongozi wa Dini kuomba dua
Baadhi ya wanafunzi wakiomba dua
Baadhi ya wananchi wakimuombea dua Hayati Magufuli
Viongozi wa CCM Mkoa wa Dodoma wakiungana na viongozi wengine kumuombea dua Hayati John Magufuli.



Wananchi wakifurahia moja ya mada iliyotolewa na viongozi wa dini wakati wa kongamano hilo

Kiongozi wa Dini, Azim Dewji akitoa mada wakati wa kongamano hilo.
Sehemu ya umati ukishiriki kwenye kongamano hilo.


Baadhi ya viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama.

Mkuu wa Dayosisi ya  Mashariki na Pwani wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Dkt. Alex Malasusa (kushoto), akijadiliana jambo na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Tanzania Bara, Rodrick Mpogolo na Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi. Askofu Malasusa  alikuwa muongozaji wa kongamano hilo.

Askofu Dkt. Ranwell Mwanisongole
Rais Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa kongamano hilo ambapo aliwashukuru viongozi wa Dini kwa kuandaa Kngamano hilo la kumuombea Rais wa Awamu ya Tano Hayati John Magufuli.Picha zote na Richard Mwaikenda
Mtoto mkubwa wa Hayati John Magufuli, Joseph akitoa shukrani kwa viongozi wa dini kuandaa kongamano hilo  kumuombea dua baba yake, lakini pia alitoa shukrani kwa viongozi wa juu na watanzania kwa ujumla walivyoshiriki kwenye kongamano hilo pamoja na mazishi.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Dodoma, Ahidi Sinene (aliyevaa koti jeusi) akiwa miongoni mwa viongozi wa CCM waliohudhuria kongamano hilo la kumuombea dua Hayati Magufuli.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages