Prince Philip
Mume wa Malikia Elizabeth II wa Uingereza Mwanamfalme Philip amefariki Dunia leo, Aprili 9, 2021 akiwa na umri wa miaka 99.
Tangazo kutoka Kasri ya Buckingham linaeleza: " Ni kwa masikitiko makubwa, Malkia ametangaza kifo cha mumewe mpenzi, Mwanamfalme Philip, Duke wa Edinburgh.
"Mwanamfalme Philip amefariki kwa amani asubuhi ya leo katika Kasri la Windsor."
Prince Philip alimuoa Bintimfalme Elizabeth mnamo 1947, miaka mitano kabla ya kuwa Malkia, na alikuwa mwenza wa mfalme ama malkia aliyehudumu kwa muda mrefu katika historia ya Uingereza.
Walikuwa na watoto wanne, wajukuu wanane na vitukuu 10.
Mtoto wao wa kwanza, Mwanamfalme Charles, alizaliwa mwaka 1948, akifuatiwa na dada yake, Bintimfalme Anne mwaka 1950.
Kufuatia kifo hicho, Rais Samia Suluhu Hassan amemtumia salam za pole, Malikia Elizabeth II kufuatia msiba huo.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇