LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Apr 30, 2021

MKUTANO MKUU MAALUMU WA CCM ULIVYORINDIMA DODOMA

Mwenyekiti mpya wa CCM, Rais Samia Suluhu Hassan akionesha tuzo aliyozawadiwa  na Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT-CCM) baada ya kuchaguliwa kwa asilimia mia moja na wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalumu kwenye Ukumbi wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa CCM, Rais Samia akikabidhiwa tuzo maalumu na Mwenyekiti wa UWT, Dkt. Gaudentia Kabaka kwa kumpongeza kwa kushinda kwa kishindo katika uchaguzi huo uliofanyika kwenye ukumbi wa Jakaya Kikwete, jijini Dodoma. 
Mmoja wa wajumbe akionesha picha maalumu ya Mwenyekiti mpya wa CCM, Rais Samia Suluhu Hassan baada ushindi kutangazwa.
Mama Salma Kikwete Mbunge wa Jimbo la Mchinga, mke wa Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete akiungana na wajumbe wenzake wa Mkoa wa Lindi kushangilia ushindi wa Mwenyekiti wa CCM, Mama Samia.
Rais Samia Suluhu Hassan akijipigia kura ya kuwa mwenyekiti.

Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Visiwani, Dkt. Ali Mohamed Shein akipiga kura ya kumchagua Mwenyekiti wa CCM, Rais Samia Suluhu Hassan.

Wajumbe wa mikoa mbalimbali wakishangilia na kucheza muziki uliokuw ukiporomoshwa na Kikundi cha TOT baada ya  kutangazwa  Rais Samia kuwa mshindi wa uenyekiti wa CCM  na kuwa Mwenyekiti wa kwanza Mwanamke.


Makatibu wakuu wastaafu wa CCM,Wilson Mkama (kushoto), Abdulrahman Kinana (katikati) na Ali Bashiru wakiwa na Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Anne Makinda na Spika mstaafu wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Ameir Pandu Kificho kwenye mkutano huo

Wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalumu wakiwa wamepagawa na wimbo wa kikundi cha TOT.

Wajumbe  wakinyoosha mikono juu kukubali kumpigia kura Mama Samia.
Wajumbe wakitumbukiza kura zao kwenye kisanduku wakati wa kumpigia kura Mama Samia.
Mmoja wa wajumbe akionesha karatasi la kumpigia kura Mama Samia kuwa Mwenyekiti.
Wakijiandaa kwenda kukusanya kura
Mbunge wa Bumbuli, Januari Makamba (kushoto) akijadiliana jambo na Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye wakati wa mkutano mkuu maalumu.
Mbunge wa Jimbo la Ilemela ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angeline Mabula (wa Tatu kulia)  akiwa na wajumbe wenzake  kutoka mkoa wa Mwanza wakati wa Mkutano huo mkuu Maalumu wa CCM.
Mbunge wa Jimbo la Mwanga, Joseph Tadayo (aliyevaa shati la kijani)  akiwa na wajumbe wenzake kutoka Mkoa wa Kilimanjaro  wakati wa Mkutano huo Mkuu Maalumu wa CCM wakati wa kumchagua Rais Samia kuwa Mwenyekiti wa sita wa chama hicho.
Ilikuwa ni furaha baada ya Mama Samia kuchaguliwa kwa kishindo kuwa Mwenyekiti
Spika wa Bunge ambaye pia ni Mjumbe wa Mkutano Mkuu, Job Ndugai akitangaza matokeo ya ushindi wa Rais Samia kuwa Mwenyekiti wa sita wa CCM.
Baadhi ya maofisa wa CCM wakiwa kwenye mkutano huo
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Lindi, Seleman Mathew akitangaza kujiunga na CCM wakati wa mkutano huo.
Aliyekuwa Mwenyekiti Kanda ya Kati na Mjumbe wa Kamati Kuu Lazaro Nayarandu akitangaza kurejea CCM wakati wa mkutano huo.

Rais mstaafu wa Awamu ya Nne,  Jakaya Kikwete akikumbatiana kwa fura na Lazaro Nyarandu ambaye alitangaza kurejea CCM kutoka Chadema ambako alikuwa  Mwenyekiti Kanda ya Kati na Mjumbe wa Kamati Kuu. 

Wajumbe wa Mkutano Mkuu wakifuatilia yanayojiri kwenye mkutano huo
Wajumbe wakitoka nje ya ukumbi baada ya mkutano huo kumalizika.
Aliyekuwa Katibu Mwenezi wa CCM, Humphrey Polepole akitangaza Sekretarieti mpya ya CCM akiwemo Katibu Mkuu mpya wa CCM, Daniel Chongolo. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA.


 

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages