Maafisa wa usalama nchini Iran wametangaza kumkamata jasusi wa utawala wa Israel katika mkoa wa Azerbaijan Mashariki katika eneo la kaskazini magharibi mwa nchi.
Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama katika mkoa wa Azerbaijan Mashariki amesema jasusi huyo wa utawala wa Israel na majasusi kadhaa wa nchi zingine wamekamatwa katika oparesheni ya maafisa wa usalama mkoani humo.
Akizungumza na waandishi habari Jumatatu, amesema hakuna kundi lolote la magaidi wakufurishaji katika mkoa huo lakini hakutoa taarifa zaidi kuhusu idadi ya majasusi waliokamatwa au uraia wao.
Hali kadhalika amesema katika miezi ya hivi karibuni pia majasusi wengine kadhaa waliokuwa wanatumikia mashirika ya kijasusi ya kigeni wamekamatwa mkoani humo.
Agosti 2020, maafisa wa usalama wa Iran waliwakamata majasusi kadhaa wa mashirika ya kijasusi ya kigeni nchini.
Akizungumza wakati huo, afisa mwandamizi wa Wizara ya Usalama alitangaza kuwa wamesambaratisha timu tano za majasusi na kusema kukamatwa majasusi hao kulikuwa pigo kubwa kwa madola ya kibeberu duniani.
Afisa huyo alisema mashirika ya kijasusi ya kigeni yanatumia mbinu za kiwango cha juu ili kupata taarifa muhumu katika sekta mbali mbali nchini Iran hasa sekta ya za nyuklia, kijeshi, kisiasa, kiuchumi na miundo msingi.
Aliongeza kuwa majasusi hao wanatekeleza shughuli zao chini ya usimamisi wa Shirika Kuu la Kijasusi la Marekani (CIA), shirika la kijasusi la utawala wa Kizayuni wa Israel, Mossad na mashirika kadhaa ya kijasusi ya nchi za Ulaya.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇