Na Bashir Nkoromo, CCM Blog Kigamboni
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dk. Faustine Ndugulile amezitaka Mamlaka zinazohusiana na Maendeleo ya Kijamii hasa Wajasiariamali katika ngazi zote ndani na nje ya Manispaa ya Kigamboni, kuunga mkono Tamasha la 'Together as One Event' ili liweze kuwa bora zaidi kwa kuwa lina mwelekeo wa kuwasaidia Wajasiriamali, wawekezaji na wabunifu hasa wa ngazi za chini.
Dk. Faustine Ndugulie ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Kigamboni jijini Dar es Salaam, ameahidi kuunga mkono hilo ambalo limebuniwa na Mwanadada Winfrida Shonde kupitia Taasisi yake ya Winnie's Hints for Success (WHS) kwa lengo la kuinua kipato, weledi na utendaji wa Wajasiriamali, wawekezaji na wabunifu wadogo ndani na nje ya Manispaa ya Kigamboni.
Dk. Ndungulile amesema hayo, jana wakati akizungumza akiwa mgeni rasmi katika Tamasha la kwanza la Together as One Event lililofanyika jana katika Viwanja vya Mjimwema, Kigamboni jijini Dar es Salaam, ambapo katika Tamasha hilo walishiriki wajasiriamali, wawekezaji na wabunifu ambao walionyesha bidhaa na huduma zao kwenye Viwanja hivyo.
Waziri Dk. Ndugulile ameahidi kushirikiana na Viongozi ndani na nje ya Manispaa ya Kigamboni kufanya mikakati ya kuwawezesha wajasiriamali, wawekezaji na wabunifu waliopo chini ya 'Together as One Event' wanapata fursa za kushiriki Maonesho makubwa kama ya Sabasaba ambayo hufanyika mwezi Julai kila mwaka, ili waweze kutambulika zaidi na kupanua wigo wa masoko ya bidhaa zao.
"Wazo hili la Tamasha hili la Together as One Event ni nzuri sana, kwa hiyo namuomba mwanzilishi wa wazo hili, Dada Winfrida Shonde atakapoandaa tena tamasha kama hili ashirikishe kwa karibu zaidi Halmashauri ya Manispaa yetu ya Kigamboni na hata hata wadau wa nje ya Manispaa hii au Serikali kuu. Na mimi kwa kuwa ni Mbunge wa jimbo hili nitasaidia, ili kuhakikisha Tamasha linakuwa bora zaidi kuliko leo.
Lakini pia mimi na Wenzangu katika Halmashauri ya Manispaa hii tunashirikiana kuhakikisha wajarisiamali, wawekezaji na wabunifu chini ya wazo hili la Dada Winfrida wanapata nafasi ya kushiriki maonyesho ya Sabasaba, isipokuwa sharti langu kubwa ni moja tu, nataka watakaoshiriki manonyesho bidhaa zao ziwe na nembo ya Kigamboni, ziandikwe 'Made in Kigamboni', akasema Dk. Ndugulile.
Baadaye Dk. Ndugulile alitembelea mabanda mbalimbali ya wajasiriamali, wawekezaji na wabunifu na kuona huku akipata amaelezo kuhusu bidhaa au huduma mbalimbali zilizokuwa zikionyeshwa kwenye mabanda hayo ambayo baadhi yake ya yaliyokuwepo ni ya Green World, Blockchain, AndRose Disability Centre, King Natural Herbs, Ugret, GNM Cargo, Ngamia, Shamba Pub, Bicol Disign na Benki ya NMB.
Bidhaa au huduma zilizoonyeshwa ni pamoja na huduma za viwanwaji na vyakula, dawa za mitishamba zilziotengenezwa kisasa, huduma za mifungo ikiwemo mbwa na nguo za kina baba, mama na watoto.
Mapema, Winfrida alisema, Tamasha hilo amelianzisha kutokana na wazo lake ambalo ameona kwamba uwepo wa Tamasha hilo utatoa fursa kwa wajasiariamali, wawekezaaji wa kati na wadogo na wabunifu kupata nafasi ya kuonyesha bidhaa zao na pia kujitangaza zaidi ili waweke kutambulika zaidi.
Alimshukuru Waziri Dk. Ndugulile kwa kuweza kuhudhuria Tamasha hilo, akisema ujio wa Waziri huyo umemtia faraja kubwa siyo yeye tu bali pamoja na wajasiriamali, wawekezaji na wabunifu waliofika kwenye tamasha hilo.
Pamoja na Waziri Ndugulile, baadhi ya viongozi wengine waliohudhuria Tamamasha hilo ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kigamboni Henry Chaula, Meya wa Kigamboni Ernest Mafimbo na Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni Ernest Kiwale.
HABARI PICHA👇
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dk. Faustine Ndugulile ambaye pia ni Mbunge wa Kigamboni, akizungumza akiwa mgeni rasmi katika Tamasha la kwanza la 'Together as One Event 2021', lililofanyika jana katika Viwanja vya Mjimwema, Kigamboni jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Muandaaji Tamasha hilo kupitia Taasisi yake ya Kijamii ya 'Winner's Hints for Success' (WHS) Winfrida Shonde. (Picha na Bashir Nkoromo). PICHA NYINGINE ZAIDI YA 50 ZA TUKIO HILI, BOFYA👉 HAPA
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇