LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Apr 11, 2021

DK. NDUGULILE ANOGESHA TAMASHA LA 'TOGETHER AS ONE EVENT' LA MWANADADA WINFRIDA SHONDE, KATIKA VIWANJA VYA MJIMWEMA, KIGAMBONI, JANA.

Mwanzoni mwa Tamasha hilo kabla ya Mgeni rasmi  kuwasili Mbunge wa Kigamboni, Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dk. Faustine Ndugulile 👇
Mwandaaji wa Tamasha la Together as One Event Mwanadada Winfrida Shonde kupitia Taasisi yake ya Winnie's Hints for Success (WHS), akiwakaribisha washiriki na wageni mbalimbali mwanzoni mwa tamasha hilo lililofanyika jana katika Viwanja vya Mjimwema, Kigamboni, Dar es Salaam.
Mwandaaji wa Tamasha la Together as One Event Mwanadada Winfrida Shonde kupitia Taasisi yake ya Winnie's Hints for Success (WHS), akimsindikiza Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kigamboni Henry Chaula, kwenda kwenye mabanda ya maonyesho ya Wajasiriamali, Wawekezaji na wabunifu wadogo mwanzoni mwa Tamasha hilo kabla ya mgeni rasmi Mbunge wa Kigamboni, Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dk. Faustine Ndugulile kuwasili.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kigamboni Henry Chaula akiangalia bidhaa mbalimbali kwenye banda la Tanganyika Kennel Ltd ambalo linajihusisha na huduma za utunzaji mbwa ikiwemo vyakula vya wanyama hao.

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kigamboni Henry Chaula, akiwa kwenye banda la King Natural Herbs ltd.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kigamboni Henry Chaula, akimuungisha kwa kununua dawa muuzaji kwenye banda hilo la Kings Natural Herbs baada ya kuridhika na maelezo ya dawa husika.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kigamboni Henry Chaula akipata maelezo kwenye banda la Ugret la wajasiriamali wa dawa za tiba asili zilizotengenezwa kisasa.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kigamboni Henry Chaula akinunua nguo kwa mjasiriamali wa uuzaji nguo mbalimbali.
Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni Ernest Mafimbo (Wapili kushoto), akiwa kwenye banda la wafanyabiashara Shamba Pub inayojihusisha na uuzaji wa bia, vinywaji baridi na vyakula ikiwemo nyama choma za mbuzi na kuku.
Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni Ernest Mafimbo akiendelea kupatiwa maelezo na wafanyabiashara hao wa Shamba PubMwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kigamboni Henry Chaula akibadilishana mawazo na Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni Ernest Mafimbo wakiwa kwenye Tamasha hilo.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kigamboni Henry Chaula akibadilishana mawazo na Diwani wa Kata ya Mjimwema.

Baada ya Mgeni rasmi Waziri na Mbunge wa Kigamboni Dk. Ndugulile kufika kwenye Tamasha hilo👇
Mwandaaji wa tamasha hilo Winfrida Shonda akiwaonyesha eneo la kuketi, wageni wake akiwemo Mgeni rasmi Mbunge wa Kigamboni, Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dk. Faustine Ndungulile, baada ya wageni hao kuwasili.
Mbunge wa Kigamboni, Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dk. Faustine Ndugulile (kushoto) akishauriana jambo na Meya wa Manispaa ya Kigamboni Ernest Mafimbo (kulia) na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kigamboni Henry Chaula (katikati) baada ya kuwasili kwenye Tamasha hilo.
Meza kuu wakiwa wameketi kusubiri mambo yaanze rasmi
Mwandaaji wa Tamasha hilo Winfrida Shonde akifanya utambulisho na kumkaribisha Mgeni rasmi kwenye Tamasha hilo, Waziri Dk. Ndugulile.  

Utambulisho wa Wadau👇

Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Kigamboni Rehema Mwimbura akizungumza.
Mwakilishi kutoka Dorsa Decoration akizungumza.
Mwakilishi kutoka UVIWATA akizungumza.
Mwakilishi wa Bodaboda akizungumza.
Sandra Chogo wa Kampuni ya Block tech akizungumza. Blocktech ni mojawapo ya Tekinolojia mpya katija mapinduzi ya nne ya Viwanda
Mwakilishi wa Shamba Pub akizungumza
Mwakilishi wa baa ya Ngamia akizungumza
Diwani wa Mjimwema akizungumza
Meya wa Manispaa ya Kigamboni akizungumzaMwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kigamboni akizungumza

Mgeni Rasmi Dk. Ndugulile akikaribishwa Jukwaani na muandaaji wa tamasha hilo kuhutubia👇
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dk. Faustine Ndugulile na Mbunge wa Kigamboni akikaribishwa jukwaani na Mwandaaji wa Tamasha hilo Winfrida shonde kuzungumza.
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dk. Faustine Ndugulile ambaye pia ni Mbunge wa Kigamboni akizungumza na viongozi na wadau kwenye Tamasha hilo.
Mwandaaji wa Tamasha hilo Winfrida Shonde akimpeleka waziri Dk. Ndugulile kutazama maonyeshoWaziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dk. Faustine Ndugulile na Mbunge wa Kigamboni akimsikiliza kwa makini mjasriamali wa dawa za tiba asili baada ya kufika kwenye banda la mjasiriamali huyo.
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dk. Faustine Ndugulile na Mbunge wa Kigamboni akipata maelezo kutoka kwa Sandra Chogo wa Kampuni ya Blocktech Tanzania Community,
alipotembelea banda la  Kampuni hiyo.
"Unaona Kitabu hiki, humu ndimo nimeandika mambo mbalimbali kuhusu Blockchain, Bitcoin na Cryptocurrency, ambayo ni mojawapo ya teknolojia mpya za mapinduzi ya nne ya viwanda", akasema Sandra.
Kisha Sandra akamkabidhi kitabu hicho Dk. Ndugulile ambaye alikinunua wa sh, 30,000.
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dk. Faustine Ndugulile na Mbunge wa Kigamboni akitazama dawa za tiba asilia kwenye banda la King Natural Herb.
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dk. Faustine Ndugulile na Mbunge wa Kigamboni akipata maelezo kwenye banda la wajasiamali wa utaalamu wa upambaji kwenye shughuli mbalimbali
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dk. Faustine Ndugulile na Mbunge wa Kigamboni akisisitiza jambo kwenye banda la Wawekezaji wa Benki ya NMB.
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dk. Faustine Ndugulile na Mbunge wa Kigamboni akipata maelezo kwenye banda la Kampuni ya GNM Cargo ya wajasiriamali wanaojihusisha na usafirishaji mizigo ya bidhaa kutoka nchini China kuja Tanzania.
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dk. Faustine Ndugulile na Mbunge wa Kigamboni akisaini kitabu cha wageni kwenye banda hilo.
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dk. Faustine Ndugulile na Mbunge wa Kigamboni akipata maelezo kwnye banda la wajasiriamali wanaojishughulisha na uuzaji wa nguo za vitenge
Kisha akapiga nao picha ya ukumbusho.
Muandaaji wa Tamasha hilo Winfrida Shonde akionyesha kitabu cha Ukombozi wa Fikra ambacho amekitunga ili kuwasaidia wajasiriamali mbalimbali kujikomboa kwa njia ya kuzifanyia kazi fikra.
Kisha akamkabidhi kitabu hicho Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dk. Faustine Ndugulile na Mbunge wa Kigamboni.

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dk. Faustine Ndugulile na Mbunge wa Kigamboni akiwa kwenye banda la Wajasiriamali waliowekeza katika biashara ya kuuza vinywaji baridi, bia na vyakula ikiwemo nyama choma na kuku.
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dk. Faustine Ndugulile na Mbunge wa Kigamboni akizungumza na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kigamboni Henry Chaula baada ya kukagua mabanda ya maonyeshoWaziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dk. Faustine Ndugulile na Mbunge wa Kigamboni akibadilishana mawazo na viongozi mbalimbali baada ya kukagua mabanda ya wajasiriamali.

Shughuli ikamalizika kwa picha mbalimbali za ukumbusho👇





Kujua alichosema Dk. Ndugulie kwenye Tamasha hilo. Bofya👉 HAPA


Maelezo/Picha zote na Bashir Nkoromo, Mwendeshaji Mkuu wa Blog ya Taifa ya CCM. 

Haki zote zimehifadhiwa, Hairuhusiwi kunakili, kusambaza au kufanyia matumizi mengine habari au picha zilizomo humu bila Idhini ya Mwendeshaji Mkuu wa Blog hii. Kwa Maulizo, ushauri au Maoni Wasiliana na nasi kwa Namba 0789 498008, au 0712 498008

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages