LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Apr 4, 2021

DK. MPANGO AWATAKA WATANZANIA KUFANYAKAZI KWA BIDII NA WELEDI WAKIMTANGULIZA MUNGU

Makamu wa Rais Dk. Philip Mpango akizungumza leo mjini Dodoma


Dodoma, Tanzania

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. Philip Isdor Mpango amewataka Watumishi wote wa Umma na Watanzania kufanya kazi kwa Bidii, Uadilifu na weledi pamoja na  kumtanguliza Mwenyezi Mungu.


Makamu wa Rais Dkt. Mpango ameyasema hayo leo April 04,2021 katika Ibada ya Misa Takatifu ya kuadhimisha Sikukuu ya Pasaka iliyofanyika katika Kanisa Kuu Katoliki Jimbo Kuu la Dodoma.


Aidha Makamu wa Rais Dkt. Philip Isdor Mpango ameitaka Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA kukusanya kodi kwa kuzingatia sheria za Nchi na kuwaacha Wafanya Biashara wafanye Biashara zao kwa  Haki na kutowanyanyasa kwenye Biashara zao ili kuleta kodi kwa ajili ya kuweza kuwahudumia Watanzania.


katika Ibada hiyo Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Mpango pia amewasilisha salam za Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuwaomba Waumini hao na Watanzania kwa ujumla waendelee kumuombea Rais Samia na kuiombea Nchi ili iweze kuneemeka zaidi  ya hapa ambapo Rais Hayati Dkt. John Pombe Magufuli ametufikisha.


katika salamu hizo Mhe. Samia Suluhu Hassan  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anawatakia Watanzania wote heri ya Sikukuu ya Pasaka na kuendelea kufanya kazi ili kuweza kuijenga Nchi yetu ya Tanzania.


No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages