Aliyekuwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia ns Kupambana na Rushwa Dk. Edward Hisea, akipongezwa baada ya kuibuka mshindi wa Urais katika Uchaguzi wa Chama Cha Wanasheria Tanganyika (TLS), jijini Arusha.
CCM Blog, Arusha
Aliyekuwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzani (TAKUKURU) Dk. Eduward Hosea, amechanguliwa kuwa Rais mpya wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) 2021-22, katika Uchaguzi uliofanyika jana, jijini Arusha.
Akitangaza matokeo, Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi huo Charles Rwechungura alisema Dk. Hosea alipata kura 297, baada ya mchuano mkali baina yake na Wanasheria wenzake, Flaviana Charles aliyepata kura 223, Shehzada Walli kura 192, Albert Msando kura 69, na Fransis Stola kura 17, jumla ya kura zilizopigwa zikiwa 802, wakati wapiga kura waliojiandikisha wakiwa 5286.
Rwechungura pia alitangaza nafasi nyigine zilizokuwa zikigombewa ikiwemo ya Makamu wa Rais wa chama hicho ambapo Gloria Kalabamu aliibuka kidedea kwa kura 395 dhidi wa mgombea mwenzie Gidion Mandes aliyepata kura 324 huku kura 77 zikiharibika.
Baada ya matokeo kutangazwa Dk. Eduward Hosea alisema uchaguzi huo umekuwa wa haki na huru na ni uchaguzi wa kuigwa ambapo mtazamo wake kusimamia utawala wa sheria kwa kuwa na Mahakama zilizo huru na TLS huru.
“Tutasimamia utawala sheria katika maeneo moja ikiwemo ni kila mtu kuwa huru na haki katika macho ya sheria pamaja na mahakama kuwa huru ikiwa ni pamoja na kuishauri serikali na kufanya nayo kazi kwa karibu,”Alisema Hosea.
Pia aliwataka Watanzania wategemee TLS itaendelea kuwa wazi, itawajibika na kuwatetea bila kujali rangi wala sura na watapigania sheria na haki kwa lugha yao ya utu.
Mgombea aliyeshika nafasi ya pili Flaviana Charles alisema uchaguzi kuwa uchaguzi ulikuwa mzuri na haukuwa na vurugu zozote na umesha salama sasa wanakitumikia chama na taifa la Tanzania katika maeneo mbalimbali.
Aliwataka Wanasheria kuwa mfano kwa jamii katika kujitokeza kupiga kura kwani ni haki yao na sio kubaki kushabikia tu kama ilivyoonekana katika uchaguzi huo ambapo idadi ya mawaikili waliojitokeza kupiga kura ikikuwa ndogo mno ikilinganishwa na idadi ya waliojiandikisha ambayo ilikuwa ni mawaikili 5286.
Aliwataka wanawake kutokata tamaa kugombea nafasi mbalimbali kwani wanawake wana nguvu kubwa katika jamii japo kuna changamoto ila wasizipe nafasi.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇