Mgeni rasmi, Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha (kulia) akipima afya wakati wa Uzinduzi wa Programu ya Wellness katika Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi.
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Benki ya CRDB Kanda ya imezindua Programu ya Wellness kwa ajili ya kuimarisha afya ya mwili na akili kwa wafanyakazi wa Benki hiyo ili kuzuia magonjwa yasiyoambukiza ikiwemo Kisukari, magonjwa ya moyo,figo mishipa ya damu, mishipa ya fahamu, figo, saratani, kifua sugu, maradhi ya meno, selimundu na magonjwa ya akili.
Uzinduzi huo umefanyika Jumapili Aprili 10,2021 katika uwanja wa taifa uliopo katika Manispaa ya Kahama Mkoa wa Shinyanga ambapo Mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha.
Uzinduzi huo uliohudhuriwa na wafanyakazi kutoka matawi mbalimbali ya Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi inayojumuisha mikoa ya Shinyanga,Tabora,Geita na wilaya ya Sengerema uliambatana na zoezi la kupima afya na ushauri nasaha kwa wafanyakazi hao wa Benki ya CRDB sambamba na mazoezi na michezo ya kuimarisha afya ya mwili na akili.
Akizindua Programu ya Wellness, Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha aliipongeza Benki ya CRDB kwa kujali afya za wafanyakazi wake akieleza kuwa kitendo cha kujali afya ni uwekezaji mkubwa na mtaji mkubwa katika maisha ya binadamu.
“Nawapongeza Benki ya CRDB kwa kuendelea kuwa wabunifu. Kitendo cha kuwa na wafanyakazi wenye afya nzuri ni uwekezaji mkubwa. Serikali itaendelea kushirikiana nanyi kwani CRDB ni Benki Bora na yenye mchango mkubwa katika kukuza uchumi wa taifa. Wafanyakazi wa Benki ya CRDB endeleeni kufanya kazi kwa weledi na uadilifu mlionao”,alisema Macha.
Mkuu huyo wa wilaya alitumia fursa hiyo kuwakumbusha wananchi kuhusu umuhimu wa kupima afya zao badala ya kusubiri waugue ndipo waende hospitali akibainisha kuwa ukijua hali ya afya yako mapema inasaidia kuchukua hatua ikiwa ni pamoja na kufika kwenye vituo vya afya kupata huduma.
Pia, Macha aliwakumbusha wananchi kuzingatia masuala ya ulaji,unywaji na mazoezi.
"Maradhi yote yasiyo ya kuambukiza huwa yanasababishwa na utaratibu wa maisha tunayoishi, hatuna mazoea ya kufanya mazoezi, tunakaa sana ofisini, darasani, kuangalia runinga, na usafiri wa gari, kutoshiriki katika michezo, ulaji chakula usio sahihi, kula vyakula vyenye mafuta mengi, sukari na chumvi nyingi na ulaji wa vyakula vingi vya wanga tofauti na mahitaji ya mwili", alieleza Macha.
Katika hatua nyingine aliwasihi wananchi kutumia taasisi za kifedha zikiwemo Benki kuomba mikopo badala ya kuchukua mikopo umiza kutoka watu binafsi hali inayowarudisha nyuma kimaendeleo.
Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano ya Wafanyakazi Kazini wa Benki ya CRDB, Timothy Fasha amesema Benki ya CRDB imeanzisha Programu ya Wellness ili kuhakikisha kuna afya ya akili na mwili kwa wafanyakazi wa Benki hiyo ikiwa ni sehemu ya kuzuia magonjwa nyemelezi yasiyoambukizwa.
Alisema asilimia 70 ya wafanyakazi wa Benki ya CRDB ni vijana hivyo katika kulinda rasilimali hiyo, wameamua kuanzisha programu ya Wellness ambapo Benki ya CRDB imeingia mkataba na Watalaamu wa afya 'Vitality Wellness (EWP) Ltd' kwa kipindi cha mwaka mmoja ambapo kila mfanyakazi atapimwa afya yake na kupewa ushauri wa kuzingatia kwa wale watakaobainika kuwa na dalili za kuwa na magonjwa yasiyoambukiza.
“Zoezi la kupima afya na kufanya mazoezi litakuwa endelevu katika kila tawi la Benki ya CRDB nchi mzima kwani sisi tunataka kuzuia magonjwa yasiyoambukiza badala ya kutibu. Kila Tawi litaweka utaratibu wa wafanyakazi kufanya mazoezi”,amesema Fasha.
ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Programu ya Wellness katika Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi Jumapili Aprili 11,2021 katika uwanja wa taifa Manispaa ya Kahama. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Programu ya Wellness katika Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi ambapo aliipongeza Benki ya CRDB kwa kujali afya za wafanyakazi wake akieleza kuwa kitendo cha kujali afya ni uwekezaji mkubwa na mtaji mkubwa katika maisha ya binadamu.
Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano ya Wafanyakazi Kazini wa Benki ya CRDB, Timothy Fasha akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Programu ya Wellness katika Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi.
Meneja Biashara Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wagana akizungumza kwa niaba ya Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Said Pamui wakati wa Uzinduzi wa Programu ya Wellness katika Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi. Kulia ni Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha. Kushoto ni Meneja Ustawi wa Afya ya Mfanyakazi na Uwezeshaji Benki ya CRDB, Crescensia Grace Kajiru
Meneja Ustawi wa Afya ya Mfanyakazi na Uwezeshaji Benki ya CRDB, Crescensia Grace Kajiru akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Programu ya Wellness katika Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi.
Awali Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha (kulia) akipima damu wakati wa Uzinduzi wa Programu ya Wellness katika Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi iliyoambatana na zoezi la upimaji magonjwa yasiyo ya kuambukiza, ushauri wa afya, michezo na mazoezi ya kuimarisha afya ya akili na mwili kwa wafanyakazi wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi Jumapili Aprili 11,2021 katika uwanja wa taifa Manispaa ya Kahama.
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha (kushoto) na Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano ya Wafanyakazi Kazini wa Benki ya CRDB, Timothy Fasha (kulia) wakipima presha wakati wa Uzinduzi wa Programu ya Wellness katika Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi iliyoambatana na zoezi la upimaji magonjwa yasiyo ya kuambukiza, ushauri wa afya, michezo na mazoezi ya kuimarisha afya ya akili na mwili kwa wafanyakazi wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi Jumapili Aprili 11,2021 katika uwanja wa taifa Manispaa ya Kahama.
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha (kushoto) akisikiliza maelezo kuhusu masuala ya Lishe wakati wa Uzinduzi wa Programu ya Wellness katika Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi iliyoambatana na zoezi la upimaji magonjwa yasiyo ya kuambukiza, ushauri wa afya, michezo na mazoezi ya kuimarisha afya ya akili na mwili kwa wafanyakazi wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi Jumapili Aprili 11,2021 katika uwanja wa taifa Manispaa ya Kahama.
Mfanyakazi wa Benki ya CRDB akipima urefu na uzito huku wengine wakiwa katika foleni wakati wa Uzinduzi wa Programu ya Wellness katika Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi iliyoambatana na zoezi la upimaji magonjwa yasiyo ya kuambukiza, ushauri wa afya, michezo na mazoezi ya kuimarisha afya ya akili na mwili kwa wafanyakazi wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi Jumapili Aprili 11,2021 katika uwanja wa taifa Manispaa ya Kahama.
Mfanyakazi wa Benki ya CRDB akipima urefu na uzito huku wengine wakiwa katika foleni wakati wa Uzinduzi wa Programu ya Wellness katika Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi iliyoambatana na zoezi la upimaji magonjwa yasiyo ya kuambukiza, ushauri wa afya, michezo na mazoezi ya kuimarisha afya ya akili na mwili kwa wafanyakazi wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi Jumapili Aprili 11,2021 katika uwanja wa taifa Manispaa ya Kahama.
Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga , Luther Mneney (kulia) akisikiliza ushauri wa Daktari baada ya kupima afya wakati wa Uzinduzi wa Programu ya Wellness katika Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi iliyoambatana na zoezi la upimaji magonjwa yasiyo ya kuambukiza, ushauri wa afya, michezo na mazoezi ya kuimarisha afya ya akili na mwili kwa wafanyakazi wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi Jumapili Aprili 11,2021 katika uwanja wa taifa Manispaa ya Kahama.
Wafanyakazi wa Benki ya CRDB wakiendelea kupima afya wakati wa Uzinduzi wa Programu ya Wellness katika Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi iliyoambatana na zoezi la upimaji magonjwa yasiyo ya kuambukiza, ushauri wa afya, michezo na mazoezi ya kuimarisha afya ya akili na mwili kwa wafanyakazi wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi Jumapili Aprili 11,2021 katika uwanja wa taifa Manispaa ya Kahama.
Mtaalamu wa afya akitoa elimu kuhusu magonjwa ya akili kwa wafanyakazi wa Benki ya CRDB wakati wa Uzinduzi wa Programu ya Wellness katika Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi iliyoambatana na zoezi la upimaji magonjwa yasiyo ya kuambukiza, ushauri wa afya, michezo na mazoezi ya kuimarisha afya ya akili na mwili kwa wafanyakazi wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi Jumapili Aprili 11,2021 katika uwanja wa taifa Manispaa ya Kahama.
Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi akiongoza wafanyakazi wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi wakati wa Uzinduzi wa Programu ya Wellness katika Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi iliyoambatana na zoezi la upimaji magonjwa yasiyo ya kuambukiza, ushauri wa afya, michezo na mazoezi ya kuimarisha afya ya akili na mwili kwa wafanyakazi wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi Jumapili Aprili 11,2021 katika uwanja wa taifa Manispaa ya Kahama.
Wafanyakazi wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi wakifanya mazoezi wakati wa Uzinduzi wa Programu ya Wellness yenye lengo la kuimarisha afya ya akili na mwili kwa wafanyakazi wa Benki ya CRDB.
Wafanyakazi wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi wakifanya mazoezi wakati wa Uzinduzi wa Programu ya Wellness yenye lengo la kuimarisha afya ya akili na mwili kwa wafanyakazi wa Benki ya CRDB.
Wafanyakazi wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi wakifanya mazoezi wakati wa Uzinduzi wa Programu ya Wellness yenye lengo la kuimarisha afya ya akili na mwili kwa wafanyakazi wa Benki ya CRDB.
Wafanyakazi wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi wakifanya mazoezi wakati wa Uzinduzi wa Programu ya Wellness yenye lengo la kuimarisha afya ya akili na mwili kwa wafanyakazi wa Benki ya CRDB.
Wafanyakazi wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi wakiendelea na mchezo wakati wa Uzinduzi wa Programu ya Wellness yenye lengo la kuimarisha afya ya akili na mwili kwa wafanyakazi wa Benki ya CRDB.
Mchezo wa kukimbia na maji yanayovuja ukiendelea wakati wa Uzinduzi wa Programu ya Wellness yenye lengo la kuimarisha afya ya akili na mwili kwa wafanyakazi wa Benki ya CRDB.
Mbio za magunia zikiendelea
Wafanyakazi wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi wakiendelea na mchezo wakati wa Uzinduzi wa Programu ya Wellness yenye lengo la kuimarisha afya ya akili na mwili kwa wafanyakazi wa Benki ya CRDB.
Wafanyakazi wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi wakikimbia wakati wa Uzinduzi wa Programu ya Wellness yenye lengo la kuimarisha afya ya akili na mwili kwa wafanyakazi wa Benki ya CRDB.
Wafanyakazi wa Benki ya CRDB tawi la Shinyanga wakicheza muziki wakati wa shindano la kucheza muziki kwenye Uzinduzi wa Programu ya Wellness yenye lengo la kuimarisha afya ya akili na mwili kwa wafanyakazi wa Benki ya CRDB. Washindi wa kwanza walikuwa ni Benki ya CRDB tawi la Tabora wakifuatiwa na Kahama, Kahama Social na Shinyanga na wote walipewa zawadi ya fedha taslimu
Wafanyakazi wa Benki ya CRDB tawi la Tabora wakicheza muziki wakati wa shindano la kucheza muziki kwenye Uzinduzi wa Programu ya Wellness yenye lengo la kuimarisha afya ya akili na mwili kwa wafanyakazi wa Benki ya CRDB. Washindi wa kwanza walikuwa ni Benki ya CRDB tawi la Tabora wakifuatiwa na Kahama, Kahama Social na Shinyanga na wote walipewa zawadi ya fedha taslimu
Burudani ikiendelea kwenye Uzinduzi wa Programu ya Wellness yenye lengo la kuimarisha afya ya akili na mwili kwa wafanyakazi wa Benki ya CRDB.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇