Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara, Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Moshi Kabengwe na |
Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Omari Kipanga, akizungmza wakati wa makabidhiano hayo na kuwaeleza Wathibi Ubora wa Elimu kuwa magari hayo si kwa ajili ya starehe bali kwa ajili ya kazi iliyokusudiwa.
Waziri Prof. Ndalichako akiingia kuendesha moja ya magari hayo.
Waziri Ndalichako akiendesha gari hilo huku akiwa amempakia Naibu Waziri Kipanga.
Waziri Prof. Ndalichako akimkabidhi ufunguo wa gari Mdhibiti Mkuu wa Ubora wa Shule Kanda ya Ziwa. Victor Bwindiki.
Sehemu ya magari yaliyokabidhiwa
Sehemu ya Wathibiti Ubora wa Shule na watumishi wa wizara hiyo wakishuhudia makabidhiano hayo.
Na Richard Mwaikenda, Dodoma
WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Pro. Joyce Ndalichako amekabidhi magari mapya 38 yatakayosaidia Uthibiti Ubora wa Shule nchini.
Imeandaliwa na Richard Mwaikenda Akizungumza wakati wa hafla ya ugawaji wa magari hayo jijini Dodoma leo, Prof. Ndalichako amesema kuwa magari hayo yatagawiwa kwenye halmashauri 27 zisizo na magari, Kanda 10 na gari moja litatumika katika Ofisi ya Makao Makuu ya Wizara kwa ajili ya shughuli za ufuatiliaji.
Amesema kuwa Wizara kupitia Idara ya Uthibiti Ubora wa Shule ina jukumu la kusimamia mfumo wa Uthibiti Ubora na kuifanya tathmini ya ufundishwaji katika shule na vyuo bus Ualimu na kutoka ushauri wa kitalaamu na kitaaluma wa walimu, wakufunzi na viongozi wa Elimu ilu kuinua Ubora elimu nchini.
"Suala la usafiri ni la muhimu sana katika kuwawezesha wathibiti Ubora wa Shule na Vyuo bus Ualimu kwa wakati. Kwa kutambua hilo Serikali imeendelea kuhakikisha inawawezesha kikamilifuWathibiti hao kuifanya kuifanya kazi zao ipasavyo. Imenunua magari haya na kuendelea kuyafanyia matengenezo yaliyopo," amesema Ndalichako.
Magari hayo aina ya Land cruiser Station Wagon ununuzi wake umegharimu zaidi ya sh. Bilioni 6. Pia magari mengine 12 yameshanunuliwa yatawasiri nchini Mei Mwaka huu.
Ndugu, nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii ya video Waziri Prof. Ndalichako, Naibu Waziri Kipanga wakielezea kuhusu umuhimu wa magari hayo ...
Mhariri Blog ya Taifa ya CCM
0754264203
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇