LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Mar 11, 2021

WAZIRI BITEKO AZINDUA MWONGOZO WA NAMNA BORA YA KUPIMA SAMPULI ZA MADINI+video

 WAZIRI wa Madini, Dotto Biteko akizindua rasmi Mwongozo wa namna Bora ya Upimaji Sampuli za Madini wakati wa mafunzo kwa viongozi wa Shirikisho la Vyama vya Wachimbaji Madini Tanzania (FEMATA) jijini Dodoma leo Machi 11,2021. Kulia ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania, GST, Dk. Mussa Budega. Kushoto ni Katibu Mkuu wa wizara, Profesa Simon Msanjila. Kitabu hicho kimeandikwa na watumishi wa GST.

Viongozi walio meza kuu wakiongozwa na Waziri Biteko wakionesha kitabu cha mwongozo wakati wa uzinduzi.
Maofisa GST walioandika kitau hicho cha mwongozo
Waziri wa Madini, Biteko akimkabidhi kitabu cha Mwongozo, Rais wa FEMATA, John Bina
Viongozi wa FEMATA wakikabidhiwa vitabu vya mwongozo

Baadhi ya viongozi wa FEMATA wakiwa katika mafunzo pamoja na kushuhudia uzinduzi wa mwongozo.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa GST, Dk. Mussa Budeba akitoa neno la utangulizi

Naibu Waziri wa Madini, Profesa Shukrani Manya akizungumza neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha Waziri Biteko.
Rais wa FEMATA, John Bina akizungumza wakati wa mafunzo hayo.
Waziri Biteko akizungumza wakati wa uzinduzi wa kitabu cha mwongozo na mafunzo hayo.
Waziri wa Madini, Biteko na Naibu Waziri Profesa Manya wakiwa na viongozi wa FEMATA



Na Richard Mwaikenda, Dodoma

WAZIRI wa Madini, Dotto Biteko amezindua Kitabu cha  mwongozo wa namna bora ya kupima kwenye maabara sampuli za madini  ili kuwa na uhakika wa upatikanaji wa madini hayo.

Uzinduzi huo ameufanya leo Machi 11, 2021 wakati wa mafunzo ya viongozi wa Shirikisho la Vyama vya Wachimbaji wa Madini Tanzania (FEMATA) katika Ofisi za Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania,GST, jijini Dodoma.

Mwongozo huo uliopokelewa kwa furaha na viongozi wa FEMATA, umeandikwa na wataalamu wa jiolojia ambao ni maofisa wa GST.

Waziri Biteko ameupongeza uongozi wa GST kwa ufanisi ikiwemo kuandika mwongozo huo muhimu kwa maendeleo ya wachimbaji madini nchini pamoja na utoaji wa mafunzo kwa viongozi hao kwa lengo la kuboresha sekta hiyo.

Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza clip ya video Waziri Biteko akizungumza, Naibu Waziri Profesa Shukrani Manya akielezea tabia ya udongo kuhama, Ofisa Mtendaji Mkuu wa GST, Dk Mussa Budeba akielezea umuhimu wa mwongozo huo na Rais wa Femata John Bina akiipongeza GST...


IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA 
MHARIRI WA BLOG YA TAIFA YA CCM
 0754264203

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages