LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Mar 6, 2021

WATU WASIOPUNGUA 20 WAUAWA, 30 WAJERUHIWA KATIKA MLIPUKO WA BOMU ULIOTOKEA MOGADISHU, SOMALIA

 

  • Watu wasiopungua 20 wauawa, 30 wajeruhiwa katika mripuko wa bomu uliotokea Mogadishu, Somalia

Watu wasiopungua 20 wameuawa na wengine 30 wamejeruhiwa katika shambulio la kigaidi la mripuko wa bomu lililotegwa garini ulilotokea nje ya mkahawa mmoja ulioko karibu na bandari katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu.

Kwa mujibu wa mashuhuda na chombo rasmi cha habari cha serikali moshi mkubwa ulitanda angani na milio ya risasi ilisikika baada ya shambulio hilo lililotokea usiku wa kuamkia leo.

Dokta Abdulkadir Aden, mwasisi wa shirika la utoaji huduma za magari ya kubebea wagonjwa la AAMIN amevieleza vyombo vya habari kuwa wameondoa maiti 20 na majeruhi 30 katika eneo la tukio.

Shambulio hilo la kigaidi lililofanywa na mtu aliyejitolea mhanga limetokea nje ya mkahawa wa Luul Yemeni ulioko karibu na bandari.

Mkazi wa eneo hilo Ahmed Abdullahi amesema: "Gari iliyokuwa ikiendeshwa kwa mwendo wa kasi iliripuka kwenye mkahawa wa Luul Yemeni. Nilikuwa naelekea mkahawani hapo lakini nilirudi mbio baada ya mripuko kutoa mtikisiko na moshi kutanda katika eneo."

Wanamgambo wa kundi la kigaidi la Ash-Shabaab

Japokuwa hadi sasa hakuna aliyetangaza kuhusika na shambulio hilo, lakini msemaji wa polisi ya Somalia Sadiq Ali Adan amelihusisha shambulio hilo na kundi la kigaidi la Ash-Shabaab lenye mfungamano na mtandao wa kigaidi wa al-Qaeda, ambalo hufanya mashambulio ya aina hiyo dhidi ya mji mkuu Mogadishu.

Kwa akali, jengo moja lililoko karibu na mkahawa wa Luul Yemeni, ambao ulishambuliwa pia mwaka uliopita, limeporomoka baada ya mripuko huo wa jana usiku na inahofiwa kuna watu wamekwama kwenye kifusi cha jengo hilo.

Mripuko huo wa shambulio la kigaidi ulitokea wakati wa chakula cha usiku ambapo mkahawa huo ulikuwa umejaa watu.../

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages