Wanafunzi 1,194 wa Shule za Msingi na Sekondari Mkoani Morogoro wamekatisha masomo baada ya kupata ujauzito kwa kipindi cha miaka minne kuanzia mwaka 2016 hadi 2019 huku wengi wao wakiwa ni wa Shule za Sekondari.
Akizungumza wakati wa kikao cha Kamati ya Ushauri mkoa (RCC) Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Loata Ole Sanare amesema hali hiyo ni hatari kwa Elimu Morogoro kwani idadi hiyo ni kubwa hivyo amevitaka vyombo vinavyohusika kuhakikisha vinasimamia changamoto ya udhibiti wa ujauzito ikiwemo kuwafikisha Mahakamani watuhumiwa.
“Serikali inatumia gharama kubwa sana katika kugharamia Elimu bure hivyo idadi hii ya Wanafunzi 1194 ni kubwa haikubaliki, Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi na Maafisa Elimu simamieni maendeleo ya Watoto wa Kike mara kwa mara “- RC Sanare
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇